Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Iran yakamia Kombe la Dunia 2026

IRAN Pict

Muktasari:

  • Iran imepangwa kundi C pamoja na New Zealand, Ubelgiji na Misri, huku michezo yote ya kundi hilo ikitarajiwa kuchezwa Marekani.

TEHRAN, IRAN: SHIRIKISHO la Soka la Iran limethibitisha rasmi timu ya taifa ya nchi hiyo itashiriki mashindano ya Kombe la Dunia mwaka huu, licha ya mvutano mkubwa wa kisiasa na kijeshi unaoendelea katika Mashariki ya Kati.

Taarifa hiyo imekuja wakati kukiwa na wasiwasi mkubwa kuhusu ushiriki wa Iran kwenye mashindano hayo kufuatia mzozo unaoendelea kati yao, Marekani na Israel tangu Februari mwaka huu.

Iran imepangwa kundi C pamoja na New Zealand, Ubelgiji na Misri, huku michezo yote ya kundi hilo ikitarajiwa kuchezwa Marekani.

IRA 01

Awali, Shirikisho la Soka la Iran lilikuwa limeiomba FIFA kuhamishia mechi zake Canada au Mexico kutokana na hali ya kisiasa, lakini ombi hilo lilikataliwa.

Rais wa FIFA Gianni Infantino tayari amesisitiza Iran itaruhusiwa kushiriki mashindano hayo, licha ya kauli zinazokinzana kutoka kwa Rais wa Marekani Donald Trump kuhusu suala hilo katika wiki za hivi karibuni.

Katika taarifa yake rasmi, Shirikisho la Iran limesema hakuna nguvu yoyote ya nje inayoweza kuizuia kushiriki Kombe la Dunia ambalo imefuzu kwa uwezo wake wenyewe.

IRA 02

Rais wa Shirikisho hilo, Mehdi Taj, pia ameweka masharti kadhaa kwa ajili ya ushiriki wa timu hiyo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wachezaji na benchi la ufundi wanapatiwa visa bila matatizo, pamoja na kuheshimiwa kwa bendera na wimbo wa taifa wa Iran wakati wa mashindano.

Aidha, Taj ametaka kuwepo kwa ulinzi wa kutosha katika viwanja vya ndege, hoteli na njia za kuelekea viwanjani.

Miongoni mwa wachezaji waliotajwa kuhitaji uhakikisho wa visa ni Mehdi Taremi na Ehsan Hajsafi, ambao wamewahi kutumikia jeshi la Iran.

Iran inatarajiwa kuanza kampeni yake ya Kombe la Dunia kwa mchezo dhidi ya New Zealand Juni 15.