Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Haaland ajiweka anga jingine EPL

Muktasari:

  • Kitendo hicho kimemfanya Haaland kuungana na Harry Kane kwenye kundi hilo la mastaa matata kabisa, ambao wameweka rekodi ya kufunga idadi ya mabao yanayozidi tarakimu mbili kwenye uwanja wa nyumbani na ugenini katika Ligi Kuu England.

MANCHESTER, ENGLAND: STRAIKA, Erling Haaland amekuwa mchezaji wa pili kufunga mabao 10 nyumbani na ugenini kwa misimu mitatu tofauti kwenye mikikimikiki ya Ligi Kuu England.

Kitendo hicho kimemfanya Haaland kuungana na Harry Kane kwenye kundi hilo la mastaa matata kabisa, ambao wameweka rekodi ya kufunga idadi ya mabao yanayozidi tarakimu mbili kwenye uwanja wa nyumbani na ugenini katika Ligi Kuu England.

Kitu kizuri ni kwamba Haaland ameweka rekodi hiyo ameifikia baada ya kufunga dhidi ya Tottenham Hotspur, timu ya zamani ya straika, Kane Jumatano iliyopita. Haaland alifunga bao lake la 20 kwenye Ligi Kuu England msimu huu, mabao 10 nyumbani na 10 ugenini.

Mtambo huo wa mabao wa Norway ulifanya kama hivyo kwenye misimu miwili iliyopita kwenye Ligi Kuu England na kwa msimu uliopita, alipofunga mabao 27, mabao 10 ilikuwa kwenye uwanja wa ugenini na 17 kwenye uwanja wa nyumbani, Etihad.

Katika msimu wake wa kwanza kwenye Ligi Kuu England, mabao 14 kati ya 36 aliyofunga msimu huu alitikisa nyavu za viwanja vya ugenini.

Sambamba na hilo, Haaland amefikia pia rekodi ya straika wa zamani wa Manchester United, Ruud van Nistelrooy ya kufunga mabao 20+ kwenye Ligi Kuu England kwa misimu mitatu ya mwanzo.

Lakini, kwenye ishu ya kufunga mabao yanayoanzia tarakimu mbili nyumbani na ugenini, Kane amefanya hivyo mara tano, kwenye misimu ya 2015/16, 2016/17, 2017/18, 2020/21 na 2022/23.