Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gyokeres njia nyeupe Arsenal

Muktasari:

  • Kupitia mkurugenzi wa michezo, Deco De Souza, Barca imesema kuwa mpango wake ni kumtumia Robert Lewandowski kama mshambuliaji wa kati na si vinginevyo.

LONDON, ENGLAND

ARSENAL huenda ikapata urahisi katika mchakato wa kumsajili straika wa Sporting Lisbon, Viktor Gyokeres baada ya Barcelona kuthibitisha kuwa haina mpango wa kumsajili.

Kupitia mkurugenzi wa michezo, Deco De Souza, Barca imesema kuwa mpango wake ni kumtumia Robert Lewandowski kama mshambuliaji wa kati na si vinginevyo.

Deco pia alisema ni kweli wanamfahamu Gyokeres kama wanavyowafahamu wachezaji wengine, lakini Januari ijayo kipaumbele sio kutafuta straika.

Timu nyingi zimekuwa zikimtaka mshambuliaji huyo raia wa Sweden mwenye umri wa miaka 26 ambaye amekuwa katika kiwango bora tangu ajiunge na Sporting Lisbon msimu uliopita ambapo alifunga mabao 43 katika michuano yote.

Timu nyingi zilijaribu kumsajili katika dirisha la majira ya kiangazi mwaka huu, lakini ilishindikana na ikaelezwa zitajaribu kufanya hivyo mwakani.

Hata hivyo, Manchester United kupitia kocha mpya, Ruben Amorim, iliweka wazi kwamba haina mpango wa kumchukua Januari na Barcelona pia imethibitisha haitafanya hivyo.

Arsenal imebakia kuwa timu pekee kati ya zile zinazopewa nafasi kubwa ya kumsajili na kuna uwezekano ikamnyakua Januari ikiwa itawekeza nguvu.

Siku nne zilizopita mabosi wa Arsenal walikuwa na kikao cha kujadili mkakati wa dirisha lijalo na iliripotiwa kuwa wamefikia uamuzi wa kutofanya usajili mkubwa Januari, ingawa suala la kutokuwa na ushindani mkubwa huenda likabadilisha uamuzi wao.

Gyokeres ambaye mkataba wake unamalizika 2028 ili kuipata huduma yake zinahitajika zaidi ya Euro 100 milioni.