Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Garnacho: Kama sio Chelsea, sichezi

GENACHO Pict

Muktasari:

  • Winga huyo wa Kiargentina, Garnacho, ambaye kwa sasa amewekwa kando na kocha Ruben Amorim anatarajia kuachana na Man United kwenye dirisha hili.

LONDON, ENGLAND: ALEJANDRO Garnacho ametuma ujumbe mzito huko Manchester United juu ya hatima yake kwenye mchezo wa soka.

Winga huyo wa Kiargentina, Garnacho, ambaye kwa sasa amewekwa kando na kocha Ruben Amorim anatarajia kuachana na Man United kwenye dirisha hili.

Lakini, sasa Garnacho anataka kwenda timu moja tu, Chelsea.

Na gwiji wa habari za usajili, Fabrizio Romano alifichua Garnacho anajiandaa kubaki Old Trafford na asicheze mechi yoyote kama hatakubaliwa uhamisho wake wa kwenda kukipiga huko Stamford Bridge.

Romano aliambia DAZN: "Ujumbe kutoka kwa mchezaji ni Chelsea au basi. Chelsea au nibaki na sichezi soka kwa miezi sita au 12 ijayo."

Romano aliongeza Chelsea imepiga hatua kubwa kwenye mazungumzo ya Garnacho baada ya kufikia makubaliano ya masilahi binafsi.

Man United awali ilipanga bei ya Garnacho kuwa Pauni 70 milioni, lakini baada ya kuona hakuna ofa yoyote iliyoletwa mezani kwa sasa kutoka Chelsea au Napoli, miamba hiyo ya Old Trafford imeshusha bei hadi Pauni 50 milioni. Garnacho aliambiwa wazi na kocha Amorim hayupo kwenye mipango yake, sambamba na wakali wengine watano ambao ni Marcus Rashford, aliyetimkia Barcelona kwa mkopo, Antony, Jadon Sancho na Tyrell Malacia.

Garnacho amekuwa akiwatibua mashabiki wa Man United kutokana na mambo yake anayofanya mtandaoni ikiwamo kuposti picha akiwa na jezi ya Aston Villa yenye Namba 9 mgongoni aliyokuwa akivaa Rashford huko Villa Park, kabla ya kuposti tena ujumbe mwingine mtandaoni baada ya Rashford kutua Barcelona.