Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Elon Musk afikiria kuinunua Liverpool

Muktasari:

  • Musk, 53, ambaye anafahamika kama Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Tesla Motors, mmiliki wa mtandao wa X (zamani Twitter) na rafiki wa karibu wa Rais Mteule wa Marekani, Donald Trump anatajwa kuwa na utajiri wa Pauni 340 bilioni.

LIVERPOOL, ENGLAND: BABA wa bilionea Elon Musk amefichua kwamba mwanaye huyo, ambaye ni tajiri Na.1 duniani anataka kuinunua klabu ya soka ya Liverpool.

Musk, 53, ambaye anafahamika kama Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Tesla Motors, mmiliki wa mtandao wa X (zamani Twitter) na rafiki wa karibu wa Rais Mteule wa Marekani, Donald Trump anatajwa kuwa na utajiri wa Pauni 340 bilioni.

Baba yake bilionea huyo, Errol, amefichua mpango huo wa Elon wakati akizungumza na Times Radio, alipoulizwa: “Je, mwanao anataka kuinunua klabu ya soka ya Liverpool?” Na alijibu: “Siwezi kusema hilo, kwa sasa ipo chini ya wamiliki Fenway Sports Group. Ndiyo, aliwahi kubainisha dhamira hiyo, lakini haina maana kwamba anataka kuinunua.”

Baba huyo wa Musk aliulizwa zaidi kama kuinunua Liverpool ni mpango uliopo kwenye akili ya mwanaye na alisema: “Angependa hilo. Ndiyo, yeyote angependa iwe hivyo. Wajukuu zake walizaliwa Liverpool, na tuna ndugu Liverpool, hivyo tuna uhusiano na Liverpool.”

Liverpool inamilikiwa na FSG tangu mwaka 2010. Forbes kwenye viwango vyao vya karibuni iliitaja Liverpool kuwa klabu namba nne duniani yenye thamani kubwa, ikithaminishwa kwa kiwango cha Pauni 4.3 bilioni.

Septemba 2023, FSG iliuza sehemu ndogo ya hisa zake kwenye kampuni ya Dynasty Equity ya Marekani. Jambo hilo liliisaidia timu hiyo kulipa madeni yake yaliyopatikana kwenye kipindi cha janga la Uviko 19, uboreshaji wa Anfield na kuununua upya uwanja wa mazoezi wa Melwood.