Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Duh! Guardiola ashtua watu

Muktasari:

  • Kocha huyo wa Manchester City anapiga hesabu za kuirudisha timu yake kwenye makali ya kushinda mechi zake msimu ujao baada ya kumaliza namba tatu na bila ya taji lolote msimu uliopita.

MANCHESTER, ENGLAND: KOCHA Pep Guardiola amewaduwaza mashabiki wa Ligi Kuu England baada ya kuibuka na mwonekano mpya kabisa katika kuelekea msimu ujao.

Kocha huyo wa Manchester City anapiga hesabu za kuirudisha timu yake kwenye makali ya kushinda mechi zake msimu ujao baada ya kumaliza namba tatu na bila ya taji lolote msimu uliopita.

Kikosi cha Man City kilitarajia kuanza mazoezi ya pre-season Jumatatu, Julai 28 baada ya mapumziko wakitokea kwenye fainali za Kombe la Dunia la Klabu.

Lakini, kocha huyo Mhispaniola aliwafanya mashabiki wake kumwangalia mara mbili mbili ili kujihakikikishia kama ni yeye kutokana na mwonekano mpya.

Guardiola, 54, sasa ameamua kupiga mwonekano wake wa kufuga ndevu na sasa amechana mustachi. Staili ambayo imekuwa gumzo mtandaoni. Shabiki wa kwanza alisema: “Ligi haijaanza tumwone bwana kipara mwenye mustachi Josep Guardiola.”

Shabiki wa pili alisema: “Huwezi tu kumposti Pep Guardiola mwenye mustachi na sisi tukae tu kimya.” Na shabiki mwingine alisema: “Ligi Kuu itatetemeka.”

Na shabiki mwingine alisema: “Pep Guardiola atakuwa ameona tangazo la msimu wa nne wa Ted Lasso, hivyo ameamua kuonyesha upendo kwa shujaa wake.”

Guardiola ameripotiwa kuwahi kuvutiwa na mustachi wa mmoja wa waandishi waliowahi kumhoji, Fred Caldeira kwamba alikuwa na mustachi uliompendeza.

Man City itacheza mechi yake ya pre-season dhidi ya Palermo, Agosti 9. Na itaanza msimu wa Ligi Kuu England kwa mechi ya ugenini kuwakabili Wolves.