Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dabi ya Prague yavunjika, mashabiki wavamia uwanja

DABI Pict

Muktasari:

  • Katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya Czech uliokuwa na ushindani mkubwa wa kuwania ubingwa, Slavia Prague walikuwa mbele kwa mabao 3-2 dhidi ya wapinzani wao Sparta Prague, jambo ambalo lilikuwa imewahakikishia taji la ligi.

PRAGUE, JAMHURI YA CZECH: MECHI kubwa ya dabi ya Jiji la Prague, Jamhuri ya Czech kati ya Slavia Prague na Sparta Prague ilisimamishwa kutokana na vurugu kubwa zilizozuka uwanjani baada ya mamia ya mashabiki kuvamia dimba wakiwa na fataki na miale ya  moto.

Katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya Czech uliokuwa na ushindani mkubwa wa kuwania ubingwa, Slavia Prague walikuwa mbele kwa mabao 3-2 dhidi ya wapinzani wao Sparta Prague, jambo ambalo lilikuwa imewahakikishia taji la ligi.

Hata hivyo, katika dakika ya saba ya muda wa nyongeza, hali ilikuwa mbaya baada ya mamia ya mashabiki wa Slavia kuingia uwanjani ghafla.

Mashabiki hao walionekana wakiwa na fataki na mwenge ya walizozirusha uwanjani, huku baadhi yao wakikaribia eneo la mashabiki wa Sparta Prague na kuelekeza fataki hizo upande wao katika tukio lililoibua taharuki kubwa.

DAB 01

Video zilizosambaa mtandaoni zilionyesha wachezaji wa timu zote mbili wakikimbia kwa hofu kuelekea kwenye handaki la kutokea uwanjani ili kujinusuru.

Kipa wa Sparta Prague, Jakub Surovcik alionekana kuanguka chini kwa maumivu baada ya kudaiwa kupigwa wakati wa vurugu hizo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Surovcik amesema kushambuliwa na kutishiwa wakati wa mechi hakukubaliki na ameahidi kufuata hatua za kisheria.

Ripoti pia zimeeleza mchezaji mwenzake Matyas Vojta pamoja na mmoja wa wahudumu wa afya wa Sparta Prague walishambuliwa katika tukio hilo.

DAB 02

Mashabiki wengine wa Slavia waliobaki majukwaani walionekana kuwakosoa wenzao walioanzisha vurugu hizo, hasa ikizingatiwa timu yao ilikuwa imesalia dakika chache tu kutwaa ubingwa.

Mwamuzi wa mchezo alisimamisha mechi hiyo kabla ya baadaye kutangaza kuahirishwa kabisa.

Sasa Slavia Prague wanaweza kuchukuliwa hatua kali na mamlaka za soka Czech na kuna hofu timu hiyo inaweza kupewa adhabu ya kupokonywa ushindi kutokana na vurugu hizo.

Mwenyekiti wa Slavia Prague, Jaroslav Tvrdik amesema amesikitishwa na yaliyotokea na walitarajia kusherehekea ubingwa pamoja na mashabiki wao, lakini hali ilibadilika baada ya wachezaji wa Sparta Prague kushambuliwa.