Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Cunha apandisha mzuka Man United

CUNHA Pict

Muktasari:

  • Staa huyo aliyesajiliwa kutoka Wolves kwenye dirisha lililopita la majira ya kiangazi alishindwa kumaliza mchezo wa ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Burnley baada ya kupatwa na maumivu ya misuli ya paja uwanjani.

MANCHESTER, ENGLAND: MATHEUS Cunha ameipa matumaini makubwa Manchester United juu ya majeraha yake yanamsumbua wakati ligi ikiwa imesimama kupisha mechi za kimataifa.

Staa huyo aliyesajiliwa kutoka Wolves kwenye dirisha lililopita la majira ya kiangazi alishindwa kumaliza mchezo wa ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Burnley baada ya kupatwa na maumivu ya misuli ya paja uwanjani.

Cunha, 26, wakati anatoka uwanjani na kuelekea kwenye korido za uwanjani Old Trafford mashabiki walikuwa na hofu kubwa kwamba huenda mchezaji huyo angekuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu.

Kocha wa Man United, Ruben Amorim alikiri kupata wasiwasi juu ya hali ya Mbrazili huyo alipozungumzwa mwishoni mwa mechi hiyo ya ushindi.

Hata hivyo, Cunha anatazamiwa kurejea uwanjani haraka kuliko ilivyotarajiwa kutokana na kile alichokiposti kwenye mtandao wa kijamii.

Staa huyo aliposti picha yake akiwa mazoezini na kuandika ujumbe wa manano manne aliposema: "Muda unakimbia kwa kasi."

Posti hiyo ilikuwa na maana kwamba kasi yake ya kupona majeraha yanayomkabili yapo juu ya kawaida. Na mashabiki waliliona hilo na kuamua kutumia kurasa zao za mitandao ya kijamii kueleza meseji zao.

Shabiki mmoja alisema: "Upone haraka."

Na mwingine aliandika: "Ninachoweza kusema hii ni ishara nzuri."

Na wa tatu alisema: "Hii ni safi sana."

Kuna shabiki alisema: "Anataka kucheza dabi kiroho mbaya."

Man United mechi yake ijayo baada ya mapumziko ya mechi za kimataifa ni Manchester derby uwanjani Etihad, Septemba 14.

Kocha Amorim anaweza kufanya mabadiliko kwenye goli lake kwa kuanza kumtumia  Senne Lammens, kipa aliyesajiliwa kutoka Royal Antwerp kwa Pauni 18 milioni na kusainishwa mkataba wa miaka mitano.

Usajili wake huo utafungua njia ya Andre Onana kuondoka Old Trafford baada ya klabu kadhaa za Uturuki kuhitaji huduma yake.