Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Colombia kuivaa Ghana, Ureno wakutane na Croatia 32 Bora

Muktasari:

  • Matokeo hayo yameifanya Colombia kumaliza kinara wa kundi ikiwa na pointi saba huku Ureno ikiwa nafasi ya pili ikiwa na pointi tano wote wakiwa hajapoteza katika hatua hiyo.

TIMU ya taifa ya Colombia imehitimisha hatua ya makundi ya Kombe la Dunia 2026 ikiwa kileleni mwa Kundi K baada ya kutoka suluhu   dhidi ya Ureno katika mchezo uliochezwa usiku wa kuamkia leo, Jumapili kwenye Uwanja wa Hard Rock  (Miami Gardens, FL).

Matokeo hayo yameifanya Colombia kumaliza kinara wa kundi ikiwa na pointi saba huku Ureno ikiwa nafasi ya pili ikiwa na pointi tano wote wakiwa hajapoteza katika hatua hiyo.

Colombia ilianza mchezo huo kwa kasi ikiongozwa na mshambuliaji Jhon Córdoba ambaye alipiga kichwa kilichopita juu kidogo ya lango kabla ya kumlazimisha Costa kufanya moja ya save bora za mchezo.

Muda mfupi baadaye, Jhon Arias alikaribia kufunga lakini mpira wake uliokolewa kwenye mstari wa goli na Ruben Neves.

Baada ya kuhimili presha hiyo, Ureno ilianza kutengeneza nafasi zake huku nahodha Cristiano Ronaldo akijaribu bahati yake kwa mpira wa adhabu wa mbali uliodhibitiwa kwa urahisi na Vargas.

Mlinda mlango huyo wa Colombia aliendelea kuwa nyota kwa kuokoa shuti la karibu la Bruno Fernandes kabla ya Joao Felix kukosa kwa kichwa  huku James Rodriguez naye akijibu kwa shuti kali lililookolewa vizuri na Costa.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ileile ambapo Felix alipoteza nafasi nyingine ya wazi kwa kupiga kichwa nje huku Jefferson Lerma akishindwa kumshinda Costa baada ya kupiga shuti lililoenda moja kwa moja mikononi mwa kipa huyo.

Kocha wa Colombia alipoingiza Richard Rios, timu hiyo iliongeza nguvu ya mashambulizi na kiungo huyo alikaribia kuifungia timu yake bao baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa James Rodriguez, lakini mpira wake ulipita nje kidogo ya lango.

Kadiri dakika zilivyosonga, Colombia ilionekana kuwa karibu zaidi kupata ushindi. Arias alimjaribu tena Costa kwa shuti lililogonga mguu wa beki kabla ya kubadili mwelekeo, lakini kipa huyo aliokoa kwa ustadi mkubwa.

Dakika za mwisho zilikuwa za presha kubwa kwa Ureno huku Colombia ikiendelea kushambulia mfululizo.

Davinson Sanchez alizamisha mpira wavuni katika muda wa nyongeza, lakini bao hilo lilikataliwa baada ya ukaguzi wa VAR kubaini alikuwa ameotea.

Sare hiyo imeifanya Colombia kuendelea kuonyesha ubora wake dhidi ya timu za Ulaya katika Kombe la Dunia, ikiwa haijapoteza ndani ya dakika 90 katika mechi zake nne zilizopita dhidi ya mataifa ya bara hilo, ikishinda mbili na kutoka sare mbili.

Kwa upande wa Ureno, matokeo hayo yameendeleza rekodi yao ya kutopoteza dhidi ya timu za Amerika Kusini katika hatua ya makundi ya Kombe la Dunia lakini hayakutosha kuwafanya wapande kileleni mwa kundi.

Kutokana na kumaliza kinara wa Kundi K, Colombia sasa itavaana na Ghana katika hatua ya 32 Bora huku Ureno ya kocha Roberto Martinez ikikumbana na Croatia katika mechi nyingine inayotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Cristiano Ronaldo alicheza dakika zote 90 akiongoza safu ya ushambuliaji ya Ureno, lakini alikabiliwa na ulinzi imara wa Colombia uliomzuia kupata nafasi nyingi za kufunga.

Kwa upande wa Colombia, James Rodriguez aliendelea kuonyesha ubora wake katika eneo la kiungo kwa kutengeneza nafasi kadhaa, huku Jhon Arias na Jhon Córdoba wakisumbua mara kwa mara ngome ya Ureno.

Baada ya kiwango alichokionyesha katika dakika 90 za mchezo huo, Santiago Arias wa Colombia alichaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Mechi (Player of the Match), akiongoza safu ya ulinzi kwa utulivu mkubwa na kusaidia timu yake kumaliza kileleni mwa kundi hilo.