Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chama la Ronaldo lachapwa nne Saudia

Riyadh. Chama la staa wa dunia Cristiano Ronaldo, Al Nassr limeanza na gundu msimu huu baada ya kulala mabao 4-1 dhidi ya wapinzani wao Al Hilal na kupoteza ubingwa wa kwanza.

Ushindi huo umewafanya Al-Hilal kutwaa ubingwa wa kwanza msimu huu wa Super Cup kwenye mchezo uliokuwa mkali na wa kuvutia kwa muda wote.

Ronaldo alianza kuifungia timu yake dakika ya 44 ya mchezo na kwenda mapumziko wakiwa wanaongoza kwa bao 1-0, lakini kipindi cha pili kilikuwa kigumu zaidi kwao.

Dakika ya 55, Sergej Milinkovic Savic aliifungia Al- Hilal bao la kusawazisha, Huku Aleksander Mitrovic akifunga mawili dakika ya 63 na 69 na bao la nne likifungwa na Malcom katika dakika ya 72 ya mchezo huo.

Ronaldo alikosa nafasi ya wazi dakika za mwisho za mchezo huo baada ya kupiga faulo iliyopaa juu ya lango.

Al Nassr walionekana kuzidiwa kwa sehemu kubwa kwenye mchezo huo baada ya kufanikiwa kupiga shuti moja tu lililolenga lango huku wapinzani wao wakipiga mashuti matano kwenye mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Prince Sultan bin Aziz.

Hii ni mara ya pili mfululizo Al-Hilal wanatwaa ubingwa huu ikiwa ni mara ya tano kwa historia na kuwa timu yenye mafanikio makubwa zaidi kwenye kombe hilo mbele ya  Al-Nassr waliotwaa mara mbili.