Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Casemiro afichua jambo

Muktasari:

  • Malacia amekuwa na msimu mbaya akikaa nje ya uwanja baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti Juni 2023.

MANCHESTER, ENGLAND: CASEMIRO amebainisha kwa nini aliamua kuigawa medali yake ya ubingwa wa Kombe la FA kwa mchezaji mwenzake wa Manchester United, Tyrell Malacia, licha ya beki huyo kutocheza dakika hata moja na hivyo kutostahili medali ya michuano hiyo.

Malacia amekuwa na msimu mbaya akikaa nje ya uwanja baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti Juni 2023.

Licha ya kutocheza hata mechi moja katika msimu uliopita, alibaki na mtazamo chanya kwenye Uwanja wa Wembley akiishuhudia timu yake ikipata ushindi 2-1 dhidi ya mahasimu wa mji mmoja Manchester City, shukrani kwa mabao ya Kobbie Mainoo na Alejandro Garnacho.

Hata hivyo, Malacia alishindwa kujiunga na wenzake katika kusherehekea kutokana na kukosekana kwake msimu mzima. Lakini Casemiro alimvuta na kumtaka awepo wakati wa kukabidhiwa kombe na hata akampa medali yake ya dhahabu ya Kombe la FA, kuhakikisha Mholanzi huyo anajisikia kuhusika katika mafanikio hayo.

“Sikujua kama Malacia amelizumgumzia hilo, lakini ni kweli, nilimpa medali yangu,” Casemiro aliwaambia wanahabari. “Hakucheza mechi hata moja msimu mzima, na hakutaka kuja kusherehekea nasi. Hapakuwa na medali kwa ajili yake, hivyo nikampa yangu. Yeye ni sehemu ya kikosi na tunamjali. Licha ya kwamba hajacheza msimu huu, tunampenda, tunamhitaji na pia anahitaji upendo.”

Man United keshokutwa Jumatano itaivaa Arsenal katika EPL kwenye Uwanja wa Emirates.