Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aubameyang ndio basi tena na Gabon

AUBA Pict

Muktasari:

  • Baada ya kupoteza mechi mbili za kwanza katika Kundi F dhidi ya Cameroon na Msumbiji, Gabon tayari walikuwa wameshaondolewa kwenye mashindano hayo na jana Jumatano walikuwa uwanjani dhidi ya mabingwa watetezi, Ivory Coast.

MARRAKECH, MOROCCO: KAZI ya kimataifa ya Pierre-Emerick Aubameyang inaonekana kumalizika kimyakimya baada ya mshambuliaji huyo kurejea Ufaransa Jumanne kutokana na majeraha, hali iliyomfanya kuikosa mechi ya mwisho wa Gabon katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025.

Baada ya kupoteza mechi mbili za kwanza katika Kundi F dhidi ya Cameroon na Msumbiji, Gabon tayari walikuwa wameshaondolewa kwenye mashindano hayo na jana Jumatano walikuwa uwanjani dhidi ya mabingwa watetezi, Ivory Coast.

Akiwa na umri wa miaka 36, ilitarajiwa kuwa mechi hiyo dhidi ya Ivory Coast ingekuwa wa mwisho katika safari yake ya miaka 16 ya kuitumikia timu ya taifa.

Hata hivyo, Aubameyang hakushiriki mechi ya mwisho ya hatua ya makundi, kwani alirudi kujiunga na klabu yake ya Olympique de Marseille.

Jeraha la paja alilopata siku chache kabla ya kuanza kwa mashindano ya Morocco liliweka shaka juu ya ushiriki wake.

AU 01

Licha ya hilo, aliingia kama mchezaji wa akiba baada ya dakika 30 katika mechi ya kwanza dhidi ya Cameroon iliyochezwa mkesha wa Krismasi na akacheza mechi nzima dhidi ya Msumbiji Jumapili, akifunga bao katika kipigo cha 3-2.

Kwa mujibu wa taarifa ya Shirikisho la Soka la Gabon iliyotolewa juzi Jumanne, vipimo vya kitabibu vilifanyika kila siku kwa kufuata taratibu za matibabu zilizokubaliwa kati ya madaktari wa Marseille na Gabon kuhusu Aubameyang.

“Tathmini ya mwisho ilithibitisha maumivu aliyokuwa nayo katika paja lake la kushoto siku moja baada ya mchezo dhidi ya Gabon na Msumbiji,” ilisema taarifa hiyo.

AU 02

“Kutokana na matokeo yasiyoridhisha yaliyomaliza safari ya Gabon mapema, jopo la madaktari kwa kushirikiana na klabu yake lilikubaliana kulinda afya ya mchezaji kwa kumwondoa katika mchezo wa mwisho usio na athari yoyote.”

Kwa muda mrefu Aubameyang amekuwa mhimili wa timu ya taifa ya Gabon, akichagua kuichezea timu hiyo aliyowahi kuichezea baba yake, licha ya kuzaliwa Ufaransa na kuichezea Ufaransa katika ngazi za vijana.

Alianza kuichezea Gabon mwaka 2009, akifunga bao dhidi ya Morocco katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia. Tangu hapo, amecheza mechi 82 za kimataifa na kufunga mabao 39.

Aubameyang aliisaidia Gabon kufika robo fainali ya AFCON walipokuwa waandaji wa mashindano hayo mwaka 2012, ingawa alikuwa mchezaji pekee aliyekosa penalti katika mikwaju ya mwisho iliyowatoa dhidi ya Mali.

AU 03

Mashindano ya Morocco yalikuwa ni mara ya sita kwake kushiriki fainali za AFCON. Mwaka 2015, alitunukiwa tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika.

Mapema mwaka huu, aliisaidia Gabon kumaliza kama moja ya timu nne bora zilizokuwa washindi wa pili katika mechi za kufuzu ushiriki wa Kombe la Dunia 2026, akifunga mabao manne katika mchezo dhidi ya Gambia mwezi Oktoba.

Hata hivyo, Gabon walishindwa katika mchujo wa Afrika mwezi uliopita, na hivyo kumaliza ndoto ya kufuzu Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza katika historia yao, litakalofanyika Amerika Kaskazini mwezi Juni.