Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal imechomoa betri kwa Garnacho

GENACHO Pict

Muktasari:

  • Winga huyo wa Man United amewekwa kando kwenye ziara za pre-season na Chelsea ilikuwa ikihitaji huduma yake kabla ya kufikiria wachezaji wengine.

LONDON, ENGLAND: HABARI ndo hiyo. Arsenal imeripotiwa kuwa na mpango wa kumsajili winga wa Manchester United, Alejandro Garnacho kabla ya kuamua kusitisha jambo hilo.

Winga huyo wa Man United amewekwa kando kwenye ziara za pre-season na Chelsea ilikuwa ikihitaji huduma yake kabla ya kufikiria wachezaji wengine.

Arsenal iliamua kwenda kumsajili winga wa Chelsea, Noni Madueke kwa ada ya Pauni 48 milioni. Na Arsenal haikuwa timu pekee iliyoamua kuachana na Garnacho kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi.

Kwa mujibu wa taarifa za kutoka Manchester, miamba Tottenham Hotspur na Atletico Madrid nazo ziliwahi kuripotiwa kumhitaji Muargentina huyo kabla ya kubadili mawazo.

Garnacho alitumikia maisha ya utotoni kwenye akademia ya Atletico kabla ya kuhamia Old Trafford na kikosi hicho cha kocha Diego Simeone kilipiga hesabu za kumrudisha kwenye mji huo alikozaliwa.

Timu hizo ziliamua kuangalia wachezaji wengine na kuachana na Garnacho, ambapo Spurs ilitumia Pauni 55 milioni kumsajili Mohammed Kudus kutoka West Ham, wakati Atletico iliwasajili Alex Baena na Thiago Almada.

Chelsea imeripotiwa kufikia makubaliano binafsi na mchezaji Garnacho na sasa mchakato umebaki kwenye kuafikiana juu ya ada ya uhamisho, huku Man United ikitaka kumuuza mchezaji huyo kabla ya dirisha kufungwa Septemba 1.

Garnacho aliripotiwa kutibuana na kocha Ruben Amorim mwishoni mwa msimu uliopita na kuambiwa atafute timu ya kwenda baada ya msimu kumalizika.