Polisi Kenya yaing'oa Coffee, sasa kuwavaa Zamalek

Muktasari:

  • Bao lililowavusha maafande hao liliwekwa kimiani na Rashid Toha raia wa Sudan Kusini katika dakika ya 19 tu ya mchezo huo na kudumu hadi filimbi ya mwisho na kusonga mbele baada ya mechi ya kwanza ikiwa nyumbani jijini Nairobi kumalizika kwa suluhu.

WAWAKILISHI wa Kenya katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, Polisi Fc imefuzu raundi ya pili ya michuano hiyo ikiwa ugenini baada ya kuing'oa Coffee Bunna ya Ethiopia kwa bao 1-0 katika mechi kali iliyopigwa kqenye Uwanja wa Abebe Bikila, jijini Addis Ababa.

Bao lililowavusha maafande hao liliwekwa kimiani na Rashid Toha raia wa Sudan Kusini katika dakika ya 19 tu ya mchezo huo na kudumu hadi filimbi ya mwisho na kusonga mbele baada ya mechi ya kwanza ikiwa nyumbani jijini Nairobi kumalizika kwa suluhu.

Hii ni mara ya kwanza kwa Polisi kushiriki michuano hiyo baada ya kunyakua Kombe la FKF maarufu kama 2024 Mozzart Bet Cup kwa mikwaju ya penalti 8-7 dhidi ya KCB na kwa matokeo hayo sasa itavaana na watetezi wa taji hilo, Zamalek ya Misri na itaanzia nyumbani kabla ya kuwafuata Wamisri jijini Cairo.

Ratiba kwa timu ya Polisi inafanana na mabingwa wa Ligi Kuu Kenya, Gor Mahia iliyofuzu raundi ya pili, kwani nao imepanwa kukutana na watetezi Al Ahly ya Misri.