Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gor Mahia yamtangaza kocha mpya Sinisa Mihic

Muktasari:

  • Mihic, mwenye umri wa miaka 48 na mwenye leseni ya UEFA Pro, atachukua nafasi ya Zedekiah ‘Zico’ Otieno ambaye alikuwa akifanya kazi kama kocha wa muda

Gor Mahia wamemtangaza kocha mpya kutoka Croatia, Sinisa Mihic, kama kocha wao mkuu.

Mihic, mwenye umri wa miaka 48 na mwenye leseni ya UEFA Pro, atachukua nafasi ya Zedekiah ‘Zico’ Otieno ambaye alikuwa akifanya kazi kama kocha wa muda baada ya kufutwa kazi kwa kocha wa zamani Leonardo Neiva kutokana na utendaji mbaya.

Zico atarudi katika nafasi yake ya awali kama kocha msaidizi pamoja na Michael Nam.

Mihic anatarajiwa kusaidia Gor Mahia kutetea taji lao la Ligi Kuu ya Kenya  (FKF-PL), ambapo kwa sasa wanashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi wakiwa na pointi 31 kutoka mechi 18 huku nafasi ya kwanza ikishikwa na Kenya Police ikiwa na pointi 37, huku Tusker pia ikiwa na pointi 37 ikishika nafasi ya pili ikitofautina idadi ya magoli ya kufunga na kufugwa

Mihic, alizaliwa katika mji wa bandari wa Rijeka, Croatia, na amejiendeleza kama kocha kupitia timu za vijana huko Croatia. Amefanya kazi katika mataifa ya Kuwait, Saudi Arabia, Libya, na Sudan.

Kituo chake cha mwisho kilikuwa ni Al-Salmiya Sporting Club cha Kuwait ambapo alifanya kazi kama kocha msaidizi kwa siku 16 tu, kutoka Februari 12 hadi Februari 28, 2022.

Amehudumu kama kocha mkuu katika klabu za NK Crikvenica (Croatia), Al-Shabaab, na Al-Fahaheel SC, na pia aliwahi kuwa kocha msaidizi wa Al-Nasr SC ya Libya na Al-Merrikh SC ya Sudan.