Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Zanzibar Heroes waalikwa Ikulu, walamba Sh50 milioni

ZNZ Pict

Muktasari:

  • Akizungumza katika Hafla Maalum ya Chakula cha Mchana aliyoiandaa kwa ajili ya Wachezaji wa Timu hiyo katika Viwanja Vya Ikulu, Rais Dk.Mwinyi ameeeleza kuwa timu hiyo imeiletea Heshima kubwa Zanzibar na Kudhihirisha Kuwa kuna Vipaji vingi vya Soka hapa nchini vinavopaswa Kuendelezwa katika Maeneo mbalimbali.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk, Hussein Ali Mwinyi ameizawadia Timu ya Taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes Tsh50 Milioni baada ya kutwaa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi 2025.

Akizungumza katika Hafla Maalum ya Chakula cha Mchana aliyoiandaa kwa ajili ya Wachezaji wa Timu hiyo katika Viwanja Vya Ikulu, Rais Dk.Mwinyi ameeeleza kuwa timu hiyo imeiletea Heshima kubwa Zanzibar na Kudhihirisha Kuwa kuna Vipaji vingi vya Soka hapa nchini vinavopaswa Kuendelezwa katika Maeneo mbalimbali.

Aidha Rais Dk.Mwinyi amefahamisha kuwa kwa mafanikio ya Zanzibar Heroes kuna kila sababu kwa Serikali Kuendelea na ujenzi wa Academy za soka kila mkoa kwa lengo la kuibua vipaji vya vijana.

Rais Dk.Mwinyi ametangaza dhamira ya kuunda kamati maalum ya kitaifa hivi karibuni itakayokuwa na jukumu la kumshauri namna bora ya kuendeleza Mpira wa Miguu visiwani humo.

Halikadhalika Rais Dk.Mwinyi ameeleza kuwa hatua za timu za Zanzibar kulibakisha Kombe la Mapinduzi kwa mwaka wa tatu mfululizo kunaashiria uwezo mkubwa wa soka na vipaji viliopo.

Rais Dk.Mwinyi ameongeza kuwa tayari wagunduzi wa vipaji vya Soka (SCOUT) wa nchini Uturuki wameonesha nia ya kwenda visiwani humo baada ya kuushuhudia mchezo wa fainali baina ya Zanzibar na Burkinafaso na kukiri Kuwepo vipaji vingi.