Z’bar Heroes kukabidhiwa bendera

Muktasari:
Timu hiyo ya visiwani inaenda katika mashindano hayo kwa lengo la kusaka ubingwa wa pili katika historia ya kombe hilo
Zanzibar. Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Zanzibar, Rashid Ali Juma leo anatarajiwa kuikabidhi bendera timu ya taifa ya Zanzibar ‘Zanzibar Heroes’ tayari kwa safari ya Kenya kwenye masshindano ya Cecafa Chalenji yatakayoanza Desemba 3, Kenya.
Afisa Habari Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), Ali Bakari ‘Cheupe’ makabidhiano hayo yanatarajiwa kufanyika ukumbi wa mapumziko wa viongozi uliopo Uwanja wa Amaan Mjini Unguja.
“Wazir atakutana na kikosi cha ‘Zanzibar Heroes’ wakati wa saa tisa alasiri ya leo, lengo ni kutoa nafasa pamoja na kuikabidhi bendera kwa kikosi hicho ambacho wakati wowote kinatarajiwa kuondoka visiwani humu kuelekea nchini Kenya”alisema.
Kikosi hicho chini ya Kocha Hemed Suleiman Morocco kinaundwa na Ahmed Ali "Salula" (Taifa ya Jang'ombe), Nassor Mrisho (Okapi), Mohammed Abdulrahman "Wawesha" (JKU), Abdallah Haji "Ninja" (Yanga), Mohd Othman Mmanga (Polisi), Ibrahimm Mohammed "Sangula" (Jang'ombe Boys), Adeyum Saleh "Machupa" (Kagera Sugar), Haji Mwinyi Ngwali (Yanga), Abubakar Ame "Luiz" (Mlandege), Issa Haidar "Mwalala" (JKU), Abdulla Kheir "Sebo" (Azam) na Ibrahim Abdallah (Taifa ya Jang'ombe), Emanuel Martin (Yanga).
Wengine ni Abdul-swamad Kassim (Miembeni City), Abdul Aziz Makame (Taifa ya Jang'ombe),Mudathir Yahya (Singida United), Omar Juma "Zimbwe" (Chipukizi), Mohd Issa "Banka" (Mtibwa Sugar), Amour Suleiman "Pwina" (JKU), Mbarouk Marshed (Super Falcon), Hamad Mshamata (Chuoni), Suleiman Kassim "Seleembe" (Majimaji), Kassim Suleiman (Prisons), Matteo Anton (Yanga), Ali Badru (Taifa ya Jang'ombe), Feisal Salum (JKU), Salum Songoro (KVZ), Khamis Mussa "Rais" (Jang'ombe boys), Mwalimu Mohd (Jamhuri), Seif Abdallah “Karihe” (Lipuli) pamoja na Ibrahim Hamad Hilika (Zimamoto).