Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga ya Msolla kuendeleza bakuli

Muktasari:

Mgombea huyo alisema pamoja na kuwa na mpango wa kuipeleka Yanga kwenye mfumo wa mabadiliko kama akipewa dhamana, wanachama nao watakuwa wakipata nafasi ya kuichangia klabu yao.

 MGOMBEA nafasi ya uenyekiti wa klabu ya Yanga, Dk Mshindo Msolla amedai kudhamiria kujenga umoja baina ya wadau na wachama mbalimbali ndani ya klabu hiyo.

Msolla ambaye aliwahi kuwa kocha wa Taifa Stars, alisema hilo kwenye uzinduzi wa kampeni zake alizofanya leo makao makuu ya klabu hiyo, Kariakoo jijini Dar es Salaam.

Mgombea huyo alisema pamoja na kuwa na mpango wa kuipeleka Yanga kwenye mfumo wa mabadiliko kama akipewa dhamana, wanachama nao watakuwa wakipata nafasi ya kuichangia klabu yao.

"Nataka kujenga umoja ndani ya klabu kwa maana ya kuirudisha timu kwa wanachi hivyo sio vibaya wenye timu kuichangia klabu yao, " alisema Msolla.

Katika jambo hilo muhimu ambalo Msolla atalisimamia alienda mbali kwa kusema pia atatengeneza mfumo wa kutoa nafasi kwa kila mwanachama kushiriki uchaguzi.

"Natambua kuwa wanachama wengi wa Yanga ambao hushiriki uchaguzi ni wale ambao wapo Dar, ndani ya uongozi wangu kama nikipewa nafasi basi wa mkoani nao watapata haki hiyo.

"Tutakuwa na mfumo ambao utawawezesha kupiga kura wakiwa kwenye matawi yao, " alisema.

VIPAUMBELE VYAKE

Msolla katika uzinduzi wa kampeni zake ameviweka wazi vipaumbele vyake vitano, vilivyobeba kauli mbiu isemayo 'Uongozi wenye mtazamo wa mabadiliko endelevu'. Vipaumbele hivyo ni:-

Kujenga umoja ndani ya klabu (kuirudisha timu kwa wananchi)

Kuendeleza mchakato wa mabadiliko ya uendeshaji wa klabu.

Kuendeleza miradi ya klabu iliyopo na kuanzisha mipya.

Kuweka misingi ya utawala bora katika uendeshaji wa klabu na kuweka misingi ya klabu kuwa na timu bora na tishio