Watatu watajwa Yanga, yumo kocha Simba

Sunday January 16 2022
watatu PIC

Msemaji wa Yanga, Haji Manara.

By Khatimu Naheka

Wakati Yanga ikitarajiwa kushuka Uwanja wa Mkwakwani kumenyana na wenyeji wao Coastal Union imefahamika kwamba kutakuwa na sapraizi kwa mashabiki wao huku majina matatu yakitajwa.

Yanga kupitia msemaji wao Haji Manara ametangaza kwamba katika mechi ya leo mbali na hesabu zao kali kusaka pointi tatu watakuwa na sapraizi kubwa kwa mashabiki wao.

Hata hivyo usiri huo umewaweka mashabiki wao katika njia panda wakigawanyika juu ya wachezaji gani watatambulishwa hii leo.

Jina la kwanza linalotajwa ni winga Mkongomani Chico Ushindi ambaye ametua jana usiku jijini Dar es Salaam.

Ushindi anayetokea TP Mazembe ya DR Congo anatua Yanga kama mchezaji wa mkopo.

Yanga imemsafirisha winga huyo ambapo inaelezwa atatambulishwa kabla ya mchezo huo kwa mashabiki wa timu hiyo.

Advertisement

Jina la pili linalotajwa katika makundi ya mashabiki wa Yanga ni mshambuliaji Simon Msuva ambaye kwasasa yupo nchini kufuatia kuwa na mgogoro na klabu yake ya Wyday Athletic ya Morocco.

Hata hivyo Msuva jana amekanusha kutokuwa na mpango wa kuhamia Yanga wala Simba akisema yeye bado ni mchezaji halali wa Wydad.

Aliyekuwa kocha wa makipa wa Simba Milton Nienov naye huenda akatambulishwa katika mchezo huo kufuatia kuwa katika watu wanaotakiwa kuongeza nguvu katika benchi la Yanga.

Nienov raia wa Brazil ameshatua nchini na hienda akatambulishwa leo akija kuchukua nafasi ya Razack Siwa ambaye anaweza kupelekwa timu ya vijana.

Advertisement