Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wachezaji Bayern washindwa kutumia tiquitaca za Pep

Muktasari:

  • Tuko katika kiwango kizuri, tuko imara, sisi ni Bayern, tunatakiwa kujitoa kwa nguvu zote katika kila mazoezi na katika kila mechi, na hiyo ndiyo njia pekee ya kupata mafanikio makubwa, kufikia kiwango cha juu ambacho ni kwa ajili ya klabu washindi wa kweli.

KATIKA toleo lililopita kwenye kitabu cha Pep Confidential, mwandishi Marti Perarnau alianza kuelezea mipango ya Kocha Pep Guardiola katika mbio za Ligi ya Mabingwa akijiandaa kuivaa Arsenal katika hatua ya 16 bora. Sasa endelea…

“Tuko katika kiwango kizuri, tuko imara, sisi ni Bayern, tunatakiwa kujitoa kwa nguvu zote katika kila mazoezi na katika kila mechi, na hiyo ndiyo njia pekee ya kupata mafanikio makubwa, kufikia kiwango cha juu ambacho ni kwa ajili ya klabu washindi wa kweli.

“Hii ni fursa ya kihistoria, sisi ni Bayern na tunahitaji kufanya kila kitu katika kuitumia fursa hii, hatutakiwi kusimama kwa wakati huu.

Ni saa 11 jioni jijini London na wachezaji ndio kwanza walikuwa wametoka kupata mlo, chini ya miti ya michikichi kwenye bustani katika Hoteli ya Landmark.

Pep alikuwa akiwasubiri katika moja ya vyumba vya mikutano vya hoteli hiyo, alikuwa mbioni kuzungumza nao mazungumzo ya kawaida ya kabla ya mechi ya ligi ya mabingwa kati ya Bayern na Arsenal, ilikuwa mechi yao ya ugenini ya hatua ya 16 bora.

Kuna mabadiliko makubwa katika kikosi kilichopangwa, Javi Martinez alicheza peke yake mbele ya mabeki wa kati na nyuma ya viungo wa kati, Lahm alirudi nafasi ya beki wa kulia na Rafinha aliwekwa benchi.

Baada ya kutangaza kikosi, Pep alianza kuzungumzia mpango wake kwenye mechi hiyo dhidi ya kikosi cha Kocha Arsene Wenger, “Jamani sote tuna uzoefu na mechi za aina hii, tumecheza mechi za mtoano za Ligi ya Mabingwa na mnajua zinavyokuwa na nini maana yake.

“Mnajua jinsi zinavyokuwa ngumu, zimejaa utata na ni mechi hatari, nataka kuwapa maelekezo maalumu.

Pep akanyamaza kidogo, kwa makusudi maalumu, kisha akaendelea, “Hiki ndicho ninachokitaka katika dakika 10 au 12 za awali, nataka mmalize mchezo kutibua hali ya kujiamini ya wachezaji wa Arsenal. Watakuja na kasi ya kutaka kushambulia, nataka mmalize mchezo.

“Chezeeni mpira kwa kupigiana pasi, kwa mara ya kwanza nataka mkifanye kile kitu ambacho nakichukia hasa, kitu ambacho nimewahi kuwaambia kuwa ni upuuzi, kitu hicho ni tiquitaca, samahani kwa hilo lakini leo nataka mlifanye hilo vizuri, kwa muda mdogo.

“Peaneni pasi bila malengo, peaneni pasi tu, mnaweza kuchoka na hilo na kuona ni zoezi lisilo na maana lakini kuna lengo katika hilo, tunataka kumiliki mpira na kuwakatisha tamaa Arsenal, wanyimeni nafasi ya kuwanyang’anya mpira, hapo wataona zile hasira zao za kutaka kuwashambulia hazina maana kwa sababu hawatakuwa na mpira wa kuwawezesha kuwasogelea.

“Hamhitaji niwaambie ni wakati gani wa kwenda mbele kuwashambulia, baada ya dakika 10 mtakapoona wanakimbia na kuishiwa nguvu wanaanza kukata tamaa na kuvunjika moyo, mtakapoona hawaufukuzii mpira kwa hasira hapo eleweni nataka muuanze uchezaji wenu.

“Hapo mnatakiwa muachane na tiquitaca na muanze kucheza soka letu, hapo ndipo mnapoanza kuwakaba koo.

Katika mechi wachezaji wake hakuna walichofanya zaidi ya kwenda tofauti na maelekezo ya Pep. Katika dakika 10 za mwanzo Bayern walipoteza mpira mara sita, hiyo ilikuwa mipira ya juu kwenye eneo la Arsenal na hivyo kuwapa wapinzani wao nafasi ya kuumiliki, je hawakufundishwa kupora mpira? Kwa nini basi waliruhusu upotee?

Kwa dakika 10 za awali, ambazo zilikuwa kama kipindi cha maisha kwa Pep, Arsenal walikuwa wakimbiakimbia, hiyo ilikuwa furaha kwa Bayern, kwa mara nyingine Manuel Neuer alikuwa kama chizi, si tu aliokoa penalti ya Mesut Ozil na michomo mingine, pia alifanya kazi ya kuwatuliza wachezaji wenzake.

Alikuwa akiwapigia kelele akiwataka wafuate maelekezo ya kocha, Neuer aliwaokoa na kuwatuliza lakini wakati huo huo kwa Pep ilikuwa ni dakika zilizojaa hasira, kocha alikuwa haelewi kulikoni wachezaji wake walikuwa wakitumia mipira mirefu na badala ya kulinda maeneo yao na kumiliki mpira kama alivyotaka.

Pia, hata uamuzi wake wa kumpanga Javi nyuma ya viungo wa kati na mbele ya mabeki nao haukufanya kazi. Kocha alishindwa kuelewa vipi ana timu ambayo imeshindwa kabisa kufuata maelekezo?

Itaendelea Jumamosi ijayo…