Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Usajili CAF… Bada, Sure Boy wapishana Yanga

BADA Pict

Muktasari:

  • Hiyo imewapa kiburi cha kuanza harakati za kufumua kikosi na kupanga hesab mpya tayari kwa mashindano hayo makubwa yanayotabiriwa kuwa na presha kubwa kwao msimu ujao.

KITAKWIMU ni rasmi kwamba Yanga imeshafuzu Ligi ya Mabingwa msimu ujao ikiwa imesaliwa na mechi kadhaa mkononi.

Hiyo imewapa kiburi cha kuanza harakati za kufumua kikosi na kupanga hesab mpya tayari kwa mashindano hayo makubwa yanayotabiriwa kuwa na presha kubwa kwao msimu ujao.

Mwanaspoti linajua kuwa viungo Salum Abubakar 'Sure Boy'na Farid Musa huenda wakapelekwa kwa mkopo Singida Black Stars kama mipango itabaki kama ilivyo sasa.

Lakini kiungo wa Singida, Josephat Arthua huenda akapishana nao ikielezwa anatarajiwa kutua Jangwani kwa msimu ujao kuongeza nguvu kwenye timu hiyo yenye nafasi kubwa ya kuleta kocha mpya mwisho wa msimu.

Watetezi hao wa Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho (FA), imejihakikishia kucheza michuano hiyo ya CAF, baada ya kukusanya pointi 70 katika mechi 26 ilizocheza hadi sasa ikiwa na uhakika wa kumaliza ndani ya nafasi mbili za juu za ligi hiyo.

BD 01

Chanzo cha kuaminika kutoka Yanga kimelimeiambia Mwanaspoti kuwa, uongozi wa timu hiyo tayari umeanza kusajili tayari kwa kujiweka mguu sawa kujifua kwa msimu mpya huku kiungo wa Singida Black Stars akiwa miongoni mwa nyota watakaocheza Yanga msimu ujao.

Staa huyo mwenye mabao matatu na asisti nane msimu huu ameanza mazungumzo na Yanga kwa ajili ya kujiunga nayo msimu ujao ataungana na Jonathan Sowah ambaye pia inaelezwa kuwa yupo katika rada za Yanga na kwa kiasi kikubwa wameshamalizana.

"Ni kweli mazungumzo ya kunasa saini ya kiungo huyo yameanza na yapo katika hatua nzuri nafikiri kama mabo yataenda sawa atakuwa sehemu ya kikosi chetu msimu ujao kama mchezaji wa ndani baada ya kubadili uraia," kilisema chanzo hicho cha habari na kuongeza:

"Tumezingatia mambo mengi kutamani kuwa na mchezaji huyo ni moja ya wachezaji walioonyesha uwezo mkubwa kwenye ligi yetu lakini pia tunaamini anaweza kuongeza nguvu kwenye kikosi chetu kutokana na aina yake ya uchezaji."

BD 02

Bada anamudu kucheza eneo la kiungo mshambuliaji namba (10) na nane kutua kwake ndani ya kikosi hicho itakuwa sehemu ya kuwa mbadala wa Stephane Aziz Ki ambaye anatajwa kuondoka ndani ya timu hiyo.

Lakini ataongeza pia kasi ya kuwania namba kikosini kama timu hiyo itafanikiwa kumbakiza Pacome Zouzoua anayecheza eneo hilo akiwa amefunga mabao nane na asisti tisa akihusika katika mabao 17 kati ya 68 yaliyofungwa na timu hiyo.

Yanga inatajwa pia ipo mbioni kumrejesha aliyekuwa kiungo wa timu hiyo, Feisal Salum 'Fei Toto' aliyepo Azam FC kwa sasa akiwa na rekodi nzuri tangu amejiunga na timu hiyo msimu uliopita.

Ukiondoa kiungo huyo sambamba na mshambuliaji waliotajwa kujiunga na Yanga timu hiyo pia ipo kwenye mazungumzo na beki wa zamani wa Simba ambaye sasa anakipiga AS FAR Henock Inonga.


SURE BOY, FARID

Wakati Bada akitajwa kuwa mbioni kuibukia Yanga, nyota viungo wawili wa timu hiyo, Farid Mussa na Salum Abubakar 'Sure Boy' hawatakuwa sehemu ya kikosi hicho kwa msimu ujao kwa kilichoelezwa kuwa watatolewa kwa mkopo dirisha kubwa la usajili kwenda Singida Black Stars.

Wawili hao wote wamebakiza mkataba wa mwaka mmoja baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili kila mmoja mwanzoni mwa msimu huu.

BD 04

Chanzo cha kuaminika kutoka Yanga kimeliambia Mwanaspoti, nyota hao wa zamani wa Azam FC, licha ya kuwa na uwezo mkubwa wanakosa nafasi ya kucheza mara kwa mara hivyo ili kulinda vipaji vyao wameona ni bora wawatoe kwa mkopo ili kwenda kuongeza ubora.

"Hadi mwisho wa msimu kila kitu kitajulikana kwasababu timu sasa inapambana kuwa na wachezaji wachache ambao wote watapata nafasi ya kucheza kulingana na ubora," alisema mtoa habari huyo na kuongeza;

"Nafasi moja inatakiwa kuwa na wachezaji wawili hadi watatu ambao wote watakuwa na ubora unaofanana ili kupishana kulingana na uhitaji wa mchezaji husika na mechi husika na sio kama ilivyo msimu mzima mechi 30 kati ya hizo mmoja anacheza 20 hadi 25 wengine wakitumika kwenye mechi tatu hadi tano."

BD 03

Mtoa taarifa huyo alisema kwasasa Yanga wanataka kuisuka ikiwa na wachezaji ambao watakuwa wanapambania nafasi na kugawana mechi bila ya kuwa na wachezaji ambao wanasubiri mmoja aumie ndio wapate nafasi ya kucheza.

Ukiondoa wachezaji hao Yanga inakibarua cha kubakiza baadhi ya wachezaji wao muhimu wa kikosi cha kwanza ambao mikataba yao inaelekea ukingoni ambao ni pamoja na Khalid Aucho, Pacome Zouzoua, Duke Abuya, Maxi Nzengeli, Attohoula Yao na wengine ambao hawana namba ya kudumu kikosi cha kwanza kama Clatous Chama, Jonas Mkude, Abuutwalib Mshery.