Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TUNATELEZA TU!

> Niyonzima wa yanga akiwatoka wachezaji wa JKT Ruvu.

Muktasari:

Kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam zimeufanya Uwanja wa Kaunda uliopo makao makuu ya Yanga, mitaa ya Twiga na Jangwani kutotamanika hali iliyowapa jeuri watani zao Simba kuwakebehi.

WAKATI Simba wakiwakejeli kutokana na uwanja wao wa Kaunda kujaa maji na matope, Yanga wamejibu mapigo kiaina kwa kuwaambia ‘nyie chongeni sisi tunateleza tu’ kwenye Ligi Kuu.

Kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam zimeufanya Uwanja wa Kaunda uliopo makao makuu ya Yanga, mitaa ya Twiga na Jangwani kutotamanika hali iliyowapa jeuri watani zao Simba kuwakebehi.

Hata hivyo Yanga imewajibu kimtindo Simba kwa kuendelea kufanya vema kwenye mechi zake za Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya jana kuwanyuka JKT Ruvu kwa mabao 3-1.

Yanga ilipata ushindi huo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mechi iliyokuwa kali na ya kusisimua ambapo JKT Ruvu itajilaumu kwa kupoteza nafasi nyingi za wazi.

Mabao ya Yanga, yalitumbukizwa kimiani na Simon Msuva dakika ya 34 kwa njia ya penalti baada ya Dickson Makwaya kuunawa mpira langoni mwake akijaribu kuokoa hatari.

Mshambuliaji Danny Mrwanda alithibitisha amerejea upya Jangwani kwa kuiandikia Yanga bao la pili dakika ya 36 akimalizia pasi murua ya Msuva, ingawa kazi kubwa ilifanywa na Mrisho Ngassa aliyewapunguza mabeki wa JKT kabla ya kutoa pasi kwa Msuva.

Sekunde chache kabla ya mapumziko, JKT Ruvu walipata bao la kufutia machozi lililofungwa na Samuel Kamuntu kutokana na kosa la kizembe la beki Juma Abdul. Kitendo hicho cha kuruhusu JKT kupata bao kilimfanya beki huyo kutaka kukunjana mashati na nahodha wake, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ wakati wakielekea vyumbani kupumzika kabla ya kuamuliwa na wenzao.

Kipindi cha pili kosa kosa ziliendelea kwa timu zote kabla ya Msuva kufunga bao la tatu na la pili kwake katika mechi hiyo.

Msuva aliye kwenye kiwango cha juu kwa sasa alifunga bao hilo dakika ya 57 akimalizia kazi nzuri ya Ngassa aliyekuwa akiwakimbiza atakavyo mabeki wa JKT Ruvu.

Kwa ushindi huo Yanga imefikisha pointi 40 katika mechi 19 na kuzidi kujikita kileleni ikimuacha bingwa mtetezi Azam kwa pointi nne wakati Simba inakamata nafasi ya tatu ikiwa na pointi 32 katika mechi 20.

VIKOSI:

Yanga: Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Mbuyu Twite, ‘Cannavaro’, Said Juma ‘Makapu’, Salum Telela/Hassan Dilunga, Harun Niyonzima/Nizar Khalfan, Danny Mrwanda/ Hussen Javu, Ngassa na Msuva.

JKT Ruvu: Benjamin Haule, Damas Makwaya, Haruna Shamte, Renatus Morris, Mohammed Fakhi, Nashon Naftal, Amos Edward/Ally Bilal, Jabir Aziz, Samuel Kamuntu, Idd Mbaga/Emmanuel Pius na Alex Abel.

MSUVA AMZIDI

KAVUMBAGU

Mabao mawili aliyofunga Msuva jana si tu yameiwezsha Yanga kubeba pointi tatu bali pia yamemfanya mchezaji huyo awe na mabao 11 ya Ligi Kuu na kumuengua Didier Kavumbagu wa Azam aliyekuwa akiongoza orodha ya wafungaji na mabao 10.