TETESI ZA USAJILI BONGO: Kakolanya katikati ya Ihefu na Namungo

Muktasari:

  • Inaelezwa kuwa, kuna maamuzi magumu yanaweza yakafanyika kwa kipa huyo baada ya kuwepo kwa taarifa za kusaini Ihefu, lakini msimu ujao huenda akacheza Namungo inayodaiwa inamtaka kwa udi na uvumba.

KIPA Beno Kakolanya aliyekuwa akiidakia Singida Fountain Gate kabla ya kujiondoa kinyemelea mwishoni mwa msimu uliomalizika hivi karibuni, inadaiwa anagombewa na Ihefu na Namungo zote za Ligi Kuu Bara.

Inaelezwa kuwa, kuna maamuzi magumu yanaweza yakafanyika kwa kipa huyo baada ya kuwepo kwa taarifa za kusaini Ihefu, lakini msimu ujao huenda akacheza Namungo inayodaiwa inamtaka kwa udi na uvumba.

Chanzo cha kuaminika kutoka Ihefu, kinaeleza kuna kigogo mmoja wa Namungo aliwapigia simu kuhitaji huduma ya kipa huyo, baada ya kujua amesaini katika timu hiyo iliyobadili jina kuwa Singida Black Stars, hivyo wapo hatua ya mazungumzo kujua namna gani ya kulimaliza jambo hilo ili kipa huyo wa zamani wa Yanga na Simba kujiunga na Wauaji wa Kusini.