Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tanzania yatoa vipigo Kriketi T20

Muktasari:

  • Michuano ya kufuzu fainali hiyo inafanyika kwenye Viwanja vya Gymkhana, jijini Dar es Salaam na Jumanne Tanzania iliibamiza Cameroon kwa wiketi tisa.

TIMU ya Taifa ya Kriketi ya Tanzania imeshinda mizunguko 20 bila upinzani mkubwa na kujiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu fainali za Kombe la Dunia.

Michuano ya kufuzu fainali hiyo inafanyika kwenye Viwanja vya Gymkhana, jijini Dar es Salaam na Jumanne Tanzania iliibamiza Cameroon kwa wiketi tisa.

Katika mchezo huo, Cameroon ndiyo iliyoanza kubeti na kutengeneza mikimbio 37 baada ya wapigaji wote 10 kutolewa kirahisi wakitumia mizunguko 12 kati ya 20.

Tanzania ilitumia mizunguko mitatu tu kuiadhibu Cameroon baada ya mikimbio 44, huku Laksh Snehal aliyeangusha wiketi nne za wapinzani alichangia kwa kiasi ukubwa ushindi huo, akisaidiana na Harsheed Chohan, Kassim Nassor, Sanjay Bon walipata wiketi mbili kila mmoja.

Jumatatu, iliishinda Lesotho kwa mikimbio 122 katika mchezo wa pili katika Uwanja wa UDSM na ndiyo iliyopata kura ya kuanza na kutengeneza mikimbio 183 na kudondosha wiketi saba baada ya kumaliza mizunguko yote 20, huku Lesotho ilifanya mikimbio 61 ikipoteza wiketi tisa.

Malawi inazidi kuonyesha ukomavu katika michuano hii baada ya kuitoa Mali kwa ushindi wa wiketi tisa, ukiwa ni ushindi wao wa tatu.

Mali ndiyo iliyoanza kubeti na kuambulia mikimbio 43 baada ya wapigaji wao wote kutolewa wakitumia mizunguko 17 kati ya 20.

Malawi ambao katika mchezo uliopita iliifunga Ghana kwa mikimbio 25, ilizivuka alama za Mali kwa kutengeza mikimbio 44, huku ikitumia mizunguko mitatu kati ya 20.

Cameroon ambao bado haijaonyesha makali, ilionja ladha ya ushindi kwa kuifunga Mali kwa wiketi sita, baada ya kutengeneza mikimbio 58, huku ikipoteza wiketi nnebaada ya mizunguko 8.5 kati ya 20.

Mali ambayo imepoteza michezo yake yote, ndiyo iliyoanza kubeti na kutengeneza mikimbio 57 baada ya wapigaji wote 10 kutolewa wakitumia mizunguko 16 kati ya 20.

Michuano hii itamalizika baada ya michezo ya tano ya kuamua mshindi wa jumla aliyeshinda mechi nyingi.