Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Taifa Stars: Miezi 12 pointi 14

Taifa Stars

Muktasari:

Tangu mwaka huu uanze, Stars imekuwa kama ina homa ya vipindi na joto la kupanda na kushuka kutokana na matokeo mabaya inayoyapata katika mechi za kirafiki za kimataifa ambazo zipo chini ya lakenda ya Fifa, jambo ambalo linazidi kufuta ndoto za Watanzania kuiona timu yake ikitamba.

TAIFA Stars kwa sasa imeshuka katika chati ya viwango vya soka duniani ikishuka mpaka nafasi ya 112 kutoka ile ya awali 110.

Tangu mwaka huu uanze, Stars imekuwa kama ina homa ya vipindi na joto la kupanda na kushuka kutokana na matokeo mabaya inayoyapata katika mechi za kirafiki za kimataifa ambazo zipo chini ya lakenda ya Fifa, jambo ambalo linazidi kufuta ndoto za Watanzania kuiona timu yake ikitamba.

Kocha, Kim Poulsen, ndiye aliyekuwa akikinoa kikosi hicho mpaka alipotimuliwa mwanzoni mwa mwaka huu na nafasi yake kuchukuliwa na Mart Nooij ambaye anaonekana kuiharibu kabisa Stars iliyoanza kuonyesha mwelekeo mzuri.

Kama ingekuwa ni mashindano ya ligi, basi katika mechi zote za mwaka huu Stars imeshinda mechi tatu, sare tano na kufungwa mbili hivyo inafunga mwaka ikiwa na pointi 14. Lakini yenyewe imezipata pointi hizo katika mechi za kirafiki za kimataifa pamoja na za michuano ya awali ya kusaka tiketi ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon).

Stars v Namibia

Stars ikiwa chini ya kocha Poulsen ilicheza mechi hiyo ya kirafiki ambayo ilikuwa ya mwisho kwa kocha huyo ambapo ilitoka sare ya bao 1-1, bao pekee la Stars lilifungwa na Khamis Mcha ambaye soka lake la klabu analipiga Azam FC.

Mechi hiyo ilichezwa Machi, 5, katika jiji la Windhoek, Namibia. Alipotimuliwa Poulsen nafasi yake ikichukuliwa na Mart Nooij.

Stars v Malawi (The Flames)

Ikiwa imeweka kambi yake Tukuyu, jijini Mbeya, Stars ilicheza mechi yake ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Malawi ‘The Flames’, mechi hiyo ilichezwa Mei 04, Uwanja wa Sokoine jijini humo, ambapo matokeo ilikuwa 0-0. Huu ulikuwa mtihani wake wa kwanza kwa Nooij tangu alipokabidhiwa mikoba.

Mechi hiyo ilikuwa ni ya kwanza baada ya Rais wa Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF), Jamal Malinzi kuunda mkakati wa Stars Maboresho ambapo kocha Nooij aliwaongeza wazoefu kwenye kikosi chake kama Edward Charles Manyama (JKT Ruvu), Elias Maguli (Ruvu Shooting), Hassan Dilunga (Yanga), Hussein Javu (Yanga), John Bocco (Azam), Kelvin Friday (Azam), Oscar Joshua (Yanga), Nadir Haroub (Yanga) na Shomari Kapombe (Azam).

Baadaye Stars ilirudiana na Malawi iliyokuwa inakwenda kucheza Uganda, mechi hiyo iliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ikijiandaa na mechi za Afcon. Katika mchezo huo Stars ilishinda bao 1-0.

Stars v Burundi

Juni 26, Stars ilicheza mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Burundi ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Muungano, Stars iliialika Burundi kusherehekea sikukuu hiyo, mchezo huo ulichezwa Uwanja wa Taifa ambapo Stars ilifungwa mabao 3-0.

Juni, Stars ilipanda Ndege kwenda Burundi kucheza mechi ya kirafiki na timu hiyo ikiwa ni mchezo wa kirafiki wa kimataifa ambao ulikuwa kwenye kalenda na Fifa, katika mchezo huo Stars ilifungwa mabao 2-0.

Stars v Benin

Oktoba 12, Stars ilicheza mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Benin, mechi hiyo ilichezwa Uwanja wa Taifa ambapo Stars iliibuka na ushindi wa mabao 4-1, Benin ilifungwa mabao hayo ikiwa na nyota wake anayecheza Ligi Kuu England katika timu ya West Bromwich, Stephane Sessegnon.

Mabao ya Stars yalifungwa na Amri Kiemba, Juma Luizio anayecheza Zesco ya Zambia, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Thomas Ulimwengu anayecheza TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wakati bao pekee la Benin lilifungwa na Suanon Fadel.

Stars v Swaziland

Mapema mwezi uliopita Taifa Stars iliweka kambi jijini Johannesburg, Afrika Kusini. IIikuwa kambi ya mbili kujiandaa na mechi yake dhidi ya Swaziland. Mechi hiyo ilichezwa Novemba 16 katika Uwanja wa Somhololo, Swaziland na kutoka sare ya bao 1-1. Bao pekee la Stars lilifungwa na Ulimwengu. Hiyo ilikuwa ni mechi ya kirafiki ya kimaitafa ya kalenda ya Fifa.

Stars v Zimbabwe

Stars ilicheza na Zimbabwe mechi ya kwanza ya kuwania kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) ambapo Stars ilishinda nyumbani kwa bao 1-0, mechi hiyo ilichezwa Mei 18 Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, mfungaji wa bao pekee la Stars akiwa ni mshambuliaji anayekipiga Azam, John Bocco.

Wiki mbili baadaye, Stars ilisafiri mpaka Zimbabwe kwa ajili ya mechi ya marudiano ambapo ilitoka sare ya bao 2-2. Mechi hiyo ilichezwa Juni huku wafungaji wa Stars wakiwa ni beki anayecheza Yanga, Cannavaro na mshambuliaji wa TP Mazembe, Ulimwengu. Matokeo hayo yaliifanya Stars isonge mbele kucheza mchezo wa raundi ya pili dhidi ya Msumbiji.

Stars v Msumbiji

Julai 20, Stars ilicheza na Msumbuji ‘Black Mambas’ baada ya kuwatoa Zimbabwe katika mcheza wa kwanza, mechi hiyo na Msumbiji ilichezwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo timu hizo zilitoka sare ya bao 2-2.

Kwenye marudiano Agosti 3, Uwanja wa Zimpeto, Maputo Stars ilifungwa 2-1.

Bao pekee la Stars lilifungwa na mshambuliaji Mbwana Samatta wa TP Mazembe, Stars ikatolewa. Kwa mwaka huu Stars imecheza mechi nne tu za mashindano ya Afcon, nyumbani mbili na ugenini moja. Wakati mechi za kirafiki imecheza saba.