Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Straika Mbrazil kurudi hadi wiki tatu

Muktasari:

Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema, mchezaji huyo kwa sasa anaendelea vizuri na anafanya mazoezi mepesi.

MSHAMBULIAJI wa Simba,  Mbrazil Walker Da Silva anatarajia kurudi uwanjani baada ya wiki tatu.
Wilker kwa sasa anaendelea na mazoezi mepesi kwa ajili ya kukaa sawa tangu alipoumia walipokuwa kwenye mazoezi yao nchini Afrika Kusini.
Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema, mchezaji huyo kwa sasa anaendelea vizuri na anafanya mazoezi mepesi.
"Wilker anaweza kuanza kucheza kama baada ya mechi mbili kutokana na tatizo lake, "alisema Aussems.
Amesema, kupona kwa mchezaji huyo kutaongeza nguvu kwenye timu kwani kwa sasa amekuwa na mapungufu kwenye safu hiyo ya ushambuliaji.
"Straika niliyenaye kwa sasa ni Meddie Kagere jambo linalonifanya niwatumie wachezaji wengine kwenye nafasi hiyo ambayo si zao,"alisema Aussems.
Katika mazoezi hayo, Wilker alikuwa akifanya mazoezi chini ya Kocha wa viungo, Adel Zrane.