Simba yapangua ratiba Championship

Wednesday November 24 2021
simba pic

PICHA NA LOVENESS BERNARD

By Charles Abel

Mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika baina ya Simba na Red Arrows itakayochezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Novemba 28 imepelekea kusogezwa mbele kwa siku moja, mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza (Championship) baina ya vinara wa ligi hiyo DTB FC na Ndanda FC.

Taarifa iliyotolewa na DTB FC imeeleza kwamba mechi yao dhidi ya Ndanda iliyokuwa ichezwe kwenye Uwanja wa Uhuru, Jumapili Novemba 28 imepangwa kuchezwa siku moja baadaye, Novemba 29 kwenye Uwanja wa Uhuru.

"Mchezo wetu wa Championship dhidi ya Ndanda uliopangwa kuchezwa tarehe 28, Novemba katika uwanja wa Uhuru umesogezwa mbele. Mchezo huo utachezwa tarehe 29, Novemba katika uwanja wa Uhuru. Sababu za kusogezwa mbele ni kupisha mchezo wa kimataifa kati ya Simba na Red Arrows utakaochezwa tarehe 28,

Wapenzi na mashabiki wa DTB tunaomba radhi Kwa mabadiliko haya, tujitokeze Kwa wingi siku husika Kwa ajili ya kuishangilia timu yetu," ilifafanua taarifa hiyo ya DTB.

DTB inaivaa Ndanda ikiwa inaongoza msimamo wa Ligi Daraja la Kwanza na pointi zake 18 wakati wapinzani wao hao wamekusanya jumla ya pointi 10 huku wakishika nafasi ya tisa.

Advertisement