Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba yaja kivingine kimataifa

Uongozi wa Simba umetambulisha jezi mpya watakazotumia kwenye Kombe la Shirikisho Afrika kuanzia hatua ya makundi.

Simba Jumapili watacheza mechi ya kwanza hatua ya makundi kwenye kombe hilo dhidi ya Asec Mimosa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kuanzia saa 10:00 jioni.

Jezi hizo mpya wa Simba mbele zitakuwa na nembo zilizoandikwa Visit Tanzania na muonekano wa picha.

Ofisa mtendaji mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez amesema klabu hii kila mwaka inaongeza thamani si kwenye pesa tu bali kuisaidia taifa hili vyema na bahati safari hii watu wengi wanapata nafasi ya kuangalia mashindano haya kupitia njia mbalimbali.

"Kulingana na ukubwa wa mashinano ya CAF, kama klabu ya nyumbani tumeamua kupeperusha bendera ya nchi yetu kwa namna nyingine kupitia kutangaza kwenye jezi zetu ambazo tutatumia katika mashindano haya," amesema Barbara.

Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Jaji Mstaafu Thomas Mihayo amesema lazima waunge mkono michezo kwani ni sehemu moja wapo ya kukuza utalii kwani mwaka jana walifanya jambo kama hilo kupiti klabu ya Yanga pia.

"Tumeamua kufanya hivi kutangaza kupiti michezo kama Simba kwenye mashindano ya kimataifa watatutangaza kupitia jezi zilizoandikwa Visit Tanzania na sasa hivi ndio mabalozi wetu," amesema Jaji Mihayo.