Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba yaendelea kukomalia ubingwa, ikiifumua Singida

Muktasari:

  • Mabao ya Simba yalifungwa na Elie Mpanzu katika dakika ya 28 akimalizia pasi ya Anicet Oura, huku bao la pili likifungwa na Oura aliyemalizia pasi ya Mpanzu.

Simba imeendelea na harakati yake ya kuusaka ubingwa wa Ligi Kuu Bara baada ya kuichapa Singida Black Stars kwa mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa leo, Jumamosi, Juni 28, 2026 kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam.

Mabao ya Simba yalifungwa na Elie Mpanzu katika dakika ya 28 akimalizia pasi ya Anicet Oura, huku bao la pili likifungwa na Oura aliyemalizia pasi ya Mpanzu.

Ushindi huo umeifanya Simba kufikisha pointi 70 baada ya kucheza mechi 29, ikiendelea kushika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi. Timu hiyo pia imefunga mabao 53 na kuruhusu 11 pekee, rekodi inayoipa sifa ya kuwa miongoni mwa timu zenye safu imara ya ulinzi msimu huu.

Wekundu wa Msimbazi waliingia uwanjani wakihitaji pointi tatu ili kuendelea kuweka presha kwa vinara wa ligi, Yanga SC, ambao wanaongoza msimamo.

Licha ya ushindani mkali wa dakika 90, Simba ilionyesha uimara mkubwa hasa katika safu ya ulinzi iliyoongozwa na Rushine De Reuck, ambaye alikuwa na kazi kubwa ya kuondoa hatari langoni.

Singida Black Stars imeendelea kupata wakati mgumu inapokutana na Simba katika misimu ya hivi karibuni, ikiwa ni mwendelezo wa matokeo yasiyoridhisha dhidi ya wapinzani hao.

Takwimu zinaonyesha kuwa katika mechi 10 za hivi karibuni baina ya timu hizo, Simba imeshinda mara saba, Singida Black Stars ikishinda mara moja, huku mechi mbili zikimalizika kwa sare.

Licha ya ushindi huo, Simba bado inalazimika kusubiri matokeo ya mzunguko wa mwisho wa ligi, ambapo matumaini yao ya ubingwa yanategemea Yanga SC kupoteza mechi yao ya mwisho dhidi ya JKT Tanzania, itakayopigwa Juni 30 kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo.

Matokeo ya mchezo huo yatakuwa na mchango mkubwa katika kuamua bingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.