Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sh25 milioni kumrudisha Luhende Jangwani

David Luhende kushoto

Muktasari:

Yanga ilimuacha beki huyo msimu huu baada ya kugoma kusaini mkataba wa mali kauli ambapo alikwenda Mtibwa Sugar alikosaini mkataba wa mwaka mmoja ambao utamalizika mwishoni mwa msimu huu.

BEKI wa Mtibwa Sugar, David Luhende, huenda akarudi Yanga ambako wamemtengea Sh25 milioni kwa ajili ya usajili wa msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

Yanga ilimuacha beki huyo msimu huu baada ya kugoma kusaini mkataba wa mali kauli ambapo alikwenda Mtibwa Sugar alikosaini mkataba wa mwaka mmoja ambao utamalizika mwishoni mwa msimu huu.

Kiongozi mmoja wa Yanga aliliambia Mwanaspoti kuwa tayari wamezungumza na Luhende ambaye ameonyesha nia ya kukubali kurudi kwa fedha hiyo ila wanasubiri kumalizana naye ligi itakapomalizika.

Alisema kuwa mapendekezo hayo yametokana na kocha wa Yanga, Hans Pluijm ambaye amedai kuwa anahitaji beki ambaye ni mzuri kukaba na kupandisha mashambulizi huku akieleza kuwa Oscar Joshua ni mzuri kukaba ila ni mzito kupanda kusiadia mashambulizi.

“Unajua ndani ya Yanga kwa sasa anayesikilizwa kwenye usajili ni kocha tu, akisema anataka mchezaji wa aina gani basi anatafutwa huyo ama kama amemuona na kuridhika naye ndiyo huyo anayefuatilia, sasa amesema anamuhitaji Luhende, ndio maana kuna mazungumzo yanaendelea kati yetu na Luhende na ameonyesha nia ya kurudi kwa ofa tuliyompa,” alisema kiongozi huyo.

Luhende alisema bado hajafanya mazungumzo yoyote rasmi na Yanga, lakini yupo tayari kurejea klabuni hapo ama kujiunga na timu nyingine yoyote ya Ligi Kuu Bara kama itampatia maslahi mazuri na wakaafikiana.”