Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Serengeti Boys kusaka fainali AFCON U17

Muktasari:

  • Rekodi ya kwanza ambayo Serengeti Boys itaweka katika mchezo huo ambao utaanza saa 1:00 usiku katika Uwanja wa Prince Hassan Moulay jijini Rabat ni ile ya kuwa timu pekee ya taifa ya Tanzania iliyowahi kuingia hatua ya juu zaidi katika mashindano makubwa ya soka duniani.

TIMU  ya Taifa ya Vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Tanzania ‘Serengeti Boys’ itaweka rekodi mbili ikiwa itapata ushindi katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana wa umri huo (AFCON U17) leo dhidi ya Misri nchini Morocco.

Rekodi ya kwanza ambayo Serengeti Boys itaweka katika mchezo huo ambao utaanza saa 1:00 usiku katika Uwanja wa Prince Hassan Moulay jijini Rabat ni ile ya kuwa timu pekee ya taifa ya Tanzania iliyowahi kuingia hatua ya juu zaidi katika mashindano makubwa ya soka duniani.

Tayari ilifanya hivyo kwa kuingia nusu fainali na ikitinga fainali itatengeneza mlima mrefu zaidi kwa nyingine nchini kuzipanda.

Rekodi ya pili ni kuwa timu ya kwanza kutoka nchi wanachama wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kuingia katika hatua hiyo tangu jina la mashindano hayo lilipobadilishwa mwaka 2016.

Katika mchezo wa leo, Serengeti Boys hapana shaka itawategemea zaidi nyota wake wawili ambao ndio vinara katika chati ya kufumania nyavu katika mashindano hayo.

Wachezaji hao ni Dismas Athanas anayeongoza akiwa ameshapachika mabao matatu hadi sasa na Razack Mbegelendi aliye na mabao mawili.

Serengeti Boys ilifuzu hatua ya nusu fainali baada ya kuichapa Algeria kwa mikwaju ya penalti 4-2 katika mechi ya robo fainali ambayo ilimalizika kwa sare ya mabao 3-3 katika muda wa kawaida.

Misri yenyewe iliingia nusu fainali baada ya kuichapa Ivory Coast kwa mabao 4-1 katika mechi nyingine ya robo fainali.

Baada ya mechi hiyo ya Serengeti Boys dhidi ya Misri, kutakuwa na mechi nyingine ya nusu fainali uwanjani hapo itakayoanza saa 4:00 usiku baina ya wenyeji Morocco na Senegal.

Mabingwa wa mashindano hayo ataondoka na kitita cha Dola 125,000 wakati mshindi wa pili atapata Dola 90,000 huku kila timu iliyofika nusu fainali itaondoka na dola 60,000.

Hivyo Serengeti Boys kwa kufika nusu fainali imejihakikishia kuweka kibindoni mzigo wa Dola 60,000.