Senzo: Hans Poppe amefanya nijue soka la Bongo

Saturday September 11 2021
senzo pic
By Mwandishi Wetu

Mtendaji Mkuu wa Mpito Yanga, Senzo Mazingiza kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika namna alivyomfahamu na alivyofanya kazi na aliyekuwa Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi Simba, Zakaria Hans Poppe aliyefariki dunia jana Septemba 10 usiku.

Senzo kabla ya kuhamia Yanga alikuwa Mtendaji Mkuu wa Simba.

"Ni pigo kwa familia ya mpira Tanzania, Mzee Hans Poppe pumzika kwa amani. Kwa nyakati nzuri na mbaya ulisimama peke yako na ilikuwa furaha kufanya kazi na wewe. Kwa muda mfupi niliweza kuelewa soka la Bongo, asante kwa kumbukumbu, pumzika mzee,"Advertisement