Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Savio yaanza kuonyesha ubabe BDL

Muktasari:

  • Mchezo huo ulishuhudiwa na mashabiki wengi wakitaka kujua nani angeibuka na mshindi siku hiyo. 

Savio imeonyesha ukubwa wake katika Ligi ya  Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL), baada ya kuifunga  Mchenga Star kwa pointi 82-77 katika mchezo uliofanyika juzi usiku kwenye Uwanja wa Donbosco Osterbay.

Mchezo huo ulishuhudiwa na mashabiki wengi wakitaka kujua nani angeibuka na mshindi siku hiyo. 

Akizungumza na Mwanaspoti baada ya mchezo kumalizika, kocha mkuu wa Mchenga Star, Mohamedi Yusuph alisema  ulikuwa ni mzuri, lakini mipango yao ilishindwa kufua dafu mbele ya wapinzani wao.

“Kufungwa kwa timu yangu ni moja ya mchezo. Kwa kweli vijana wangu walipambana na sasa tunajipanga katika michezo inayofuata,” alisema Yusuph.

Akizungumza kuelekea kutafuta nafasi ya kucheza hatua ya nane bora, kocha huyo alisema licha ya ligi ya mwaka huu kuwa ngumu, anaamini timu yake itapambana ili kuhakikisha inacheza hatua hiyo.