Samatta ajenga msikiti Mkuranga wa waumini 5,000
Muktasari:
- Mbwana Samatta amejenga msikiti mkubwa ambao utaingiza watu 5,000 na unaweza ukatumika wakati ukarabati unaendelea.
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, anayekipiga klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji, amejenga msikiti Vikindu wilayani Mkuranga, Mkoa wa Pwani ambao unauwezo wa kuchukua watu 5,000.
Msikiti huo unaojengwa nahodha huyoo wa timu ya Taifa Tanzania ‘Taifa Stars’, kwa hatua ulipofikia sasa unaweza kutumika.
MCL Digital limefika eneo alipojenga msikiti linalojulikana Idukwa katika tarafa ya Vikindu, Kata ya Kidubwa Mkoa wa Pwani na kushuhudia ujenzi ulipofikia.
Baba mzazi wa supastaa huyo, Ally Samatta Pazi ameeleza kwamba msikiti huo unaweza kutumika kwa wahitaji wa huduma hiyo.
"Ulipofikia unaweza kutumika wakati umaliziaji ukiendelea kwani sehemu muhimu zipo tayari na maji yapo kwa wingi. "Ni msikiti mkubwa sana upande wa wanaume unachukua watu 3,000 na wanawake 2,000 utakuwa msaada kwa eneo hili," anasema.