Sababu za Newcastle kumsajili Samatta badala ya Palace

Wednesday November 13 2019
pic samagoal

Dodoma. ACHANA na kauliACHANA na kauli ya Mbwana Samatta aliyoitoa wakati alipotua jijini Dar as Salaam kwamba hajapewa taarifa na wasimamizi wake kuhusu kutakiwa na klabu za England. ya Mbwana Samatta aliyoitoa wakati alipotua jijini Dar as Salaam kwamba hajapewa taarifa na wasimamizi wake kuhusu kutakiwa na klabu za England.

Ukweli ambao unapaswa kuufahamu kuhusu taarifa za kutakiwa kwake na baadhi ya timu za Ligi Kuu England ambazo zinatajwa kuwania saini yake.

Timu hizo ni Crystal Palace, West Ham na zaidi Newcastle United ambayo ndio inamlenga zaidi Samatta kuliko timu zingine.

Kwa taarifa yako, Newcastle United kupitia wataalam wao wa ufuatiliaji wa vipaji (Maskauti) walikuwepo uwanjani Anfield wakati wa mchezo wa Liverpool dhidi ya Genk.

Katika mchezo huo mlengwa wao (Samatta) alifanikiwa kufunga bao zuri la kichwa ambalo lilimpa thamani zaidi kwa jinsi alivyofunga kwa ustadi mkubwa na kumshangaza kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp.

Kutokana na Newcastle kuwa na uhitaji mkubwa wa mshambuliaji kufuatia waliopo akiwemo Andy Carroll kushindwa kutamba ni sababu kubwa ya timu hiyo kumtaka Samatta.

Advertisement

Sababu nyingine ni ukweli kwamba kocha wa timu hiyo, Steve Bruce kumfahamu Samatta kabla hata ya kukabidhiwa kazi ya kuinoa timu hiyo aliwahi kumtaka Samatta wakati akiwa na timu ya Sheffield Wednesday ya daraja la kwanza England.

Samatta yupo nchini kuitumikia Taifa Stars katika mechi dhidi ya Guinea ya Ikweta ana mkataba unaomruhusu kung'oka Genk kwa dau la Paundi 10 milioni.

Advertisement