Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ronaldo kwa mademu balaa, Messi na Antonella wametulia tu

Muktasari:

Messi kwa upande wake alikuwa baba kwa mpenzi wake wa siku nyingi, Antonella Roccuzzo, wana umri mmoja na wote wanatokea Argentina, wamejuana tangu wakiwa na miaka mitano.

TOLEO lililopita, Mwandishi, Luca Caioli aliyachambua mambo yanayowapendeza Ronaldo na Messi nje ya soka huku akimtaja Ronaldo kupenda mchezo wa tenisi, pamoja na kuizungumzia familia ya Messi na Ronaldo. Sasa endelea…

Familia ya mama yake Ronaldo ilipata taarifa za kuzaliwa mtoto huyo kwa simu kutoka kwa mtu ambaye hawakumfahamu ambaye aliwaambia, “Nimepata mtoto na naomba nyinyi mje kunisaidia kumlea na kumlinda, katika namna ileile mliyofanya kwa wakati wote kwangu na kwa ndugu zangu, hakuna ambaye atamjua nani hasa mama mzazi,” alisema Ronaldo.

Messi kwa upande wake alikuwa baba kwa mpenzi wake wa siku nyingi, Antonella Roccuzzo, wana umri mmoja na wote wanatokea Argentina, wamejuana tangu wakiwa na miaka mitano.

Ni binamu wa rafiki wa utotoni wa Messi, Lucas Scaglia. “Nimemwona akikua naye ameniona mimi nikikua, familia zetu zinafahamiana kwa hiyo sikuwa na shaka yoyote,” alisema Messi.

Mpenzi wa Messi alisoma udaktari akibobebea katika tiba ya meno na baada ya hapo akasomea mawasiliano kabla ya kuhamia Barcelona kuishi na Messi. Septemba 11, 2015, mtoto wao wa pili, Mateo alizaliwa walionekana kuwa imara na familia yenye furaha.

Maisha ya mapenzi kwa Ronaldo yamekuwa na mambo ya kupanda na sintofahamu, vyombo vya habari mara kwa mara vimekuwa vikimhusisha na wasichana tofauti, ikiwamo orodha ya wapenzi na marafiki zake wa kike isiyo na mwisho, ni kweli au uzushi lakini hivyo ndivyo ilivyo.

Katika kundi hilo wapo wasichana warembo kutoka Uingereza, Hispania, Brazil, Colombia, Italia, Ureno Denmark na Urusi, wote hao wamekuwa wakitajwa kuwa katika uhusiano wa kimapenzi na Ronaldo kwa nyakati tofauti tofauti.

Uvumi huo uliendelea hata wakati ambao alikuwa katika miaka mitano ya uhusiano wake na Mwanamitindo, Irina Shayk, mapenzi ambayo yaliibuka baada ya kuhusishwa kupitia mitandao yao ya kijamii lakini urafiki au mapenzi hayo yalifikia mwisho ghafla Januari 2015.

Yalikuwa ni mapenzi baada ya kuonana mara ya kwanza katika onyesho la upigaji picha la Armani ingawa katika wakati wote wa uhusiano wao walikuwa wakiandamwa na uvumi wa kuwa katika misuguano ya hapa na pale.

Awali kuachana kwao kulitajwa kuwa ni wa kawaida katika jamii na sababu ilitajwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa ni utata ulioibuka kati ya mwanamitindo huyo na familia ya Ronaldo.

Hata hivyo, hatimaye, Irina aliamua kuvunja ukimya na kubainisha kwamba kuachana kwao hakukuwa jambo la kawaida kama ambavyo imekuwa ikifikiriwa siku za nyuma.

“Natafuta mwanamume ambaye ni muungwana na mwaminifu,” alisema katika mazungumzo yake na E News ambako wiki chache baadaye aliamua kufunguka zaidi katika mahojiano maalumu na ya kina na Jarida la Hola ambapo alisema alijiona asiye na maana na aliyekosa amani wakati akiwa na Ronaldo.

Kwa mara nyingine tena alisisitiza umuhimu wa kuwa na mwanamume mwaminifu na akihitimisha kwa kusema awali alidhani amempata mwanamume wa uhakika lakini kumbe haikuwa hivyo.

Wakati hayo yakiendelea, Gazeti la The Sun liliripoti Ronaldo alimsaliti, Irina kwa wasichana 12 tofauti.

Ronaldo ni tajiri, maarufu na anavutia, anafurahia kutambia mwili wake na hana mapungufu katika mbinu za ushawishi, anafahamika kama ‘mtu wa wana,’ mpenda mademu ambaye anadaiwa kuwahi kutoka na Paris Hilton japokuwa hilo linaweza kuwa ni gumzo tu la vyombo vya habari.

Hata hivyo, mwenyewe amekuwa akisisitiza anapenda kuona maisha yake binafsi yanakuwa ya siri na siyo matangazo kwa kila mtu.

“Nina kipindi cha kuwa kwenye mapenzi, hapo naweza kuwa makini mno,”

Linapokuja suala la wanawake Ronaldo anasema anapenda tabasamu zuri, mvuto wenye kuhamasisha, uungwana na mazungumzo yanayovutia.

“Kucheka ni kati ya mambo ya kunisaidia kupoteza muda,” anasema ingawa anasema hapo hapo tusisahau mwonekano mzuri jambo ambalo anasema lina umuhimu sana ingawa muhimu zaidi ni kile kilicho ndani hata kama mwanamke ana uzuri wa kipekee kama Angelina Jolie.

Itaendelea Jumanne ijayo…