Rekodi yavunjwa, Tanzania yatinga fainali

Rekodi yavunjwa, Tanzania yasonga

LICHA ya kuvunjiwa rekodi ya kutofungwa bao katika mechi yeyote kwenye michuano ya Cosafa inayoendelea huko
Afrika ya Kusini, timu ya taifa ya Tanzania Twiga Stars imefanikiwa kutinga hatua ya fainali  kwa ushindi wa penalti 3-1
mbele ya Zambia katika mchezo wa nusu fainali.
Hadi inaingia kwenye hatua hiyo Tanzania haikuwa imeruhusu bao wala kupoteza mechi katika hatua ya makundi
ambapo ilishinda mechi zote tatu na kukusanya alama tisa.
Bao la mapema la Tanzania lilifungwa kwa juhudi kubwa za beki wa kushoto  Enekia Kasonga ambaye alimpasia
Mwanahamisi aliyepiga pasi iliyozamishwa nyavuni na beki wa Zambia Lushomo Mweemba dakika ya 17.
Hata hivyo, Zambia ilisawazisha kwa makosa ya golikipa wa Twiga Janeth Simba aliyetoka mbele ya lango na kumpa
nafasi Grace Chanda kupiga shuti la umbali mrefu baada ya kuupokonya mpira kutoka kwa Fatuma Issa.
Wakati mechi inaelekea ukingoni Kocha Bakari Shime alimuingia golikipa Zubeda Mgunda kwa jukumu la kuokoa
michomo ya penalti.
Muda mchache baadae mechi ilimalizika kwa timu zote kutoshana nguvu na changamoto ya mikwaju ya penalti ilifuatia
ambapo kwa upande wa Tanzania kapteni wa U-20 Enekia Kasonga alipata penalti ya kwanza  baada Zambia kuanza
kupata kupitia Penalti ya  Elizabeth Mupeso.  
Baada ya penalti ya kwanza ufunguzi Zambia ilikosa penalti yake ya pili iliyopigwa na Margaret Belemu sawa na
Tanzania ambapo Amina Bilal alikosa.
Zambia ilipata penalti ya tatu iliyopigwa na Agness Musase sawa na Tanzania ambapo Fatuma Issa ndio alipiga.
Ubora wa Zubeda ulisababisha Zambia ishindwe kupata penalti yake ya nne iliyopigwa na Lushomo Mweemba wakati
Tanzania ilijifunga kupitia kwa Oppa Clement na mchezo ukamalizwa na Zubeda mwenyewe aliyedaka penalti ya
Zambia iliyopigwa na Lubandji Ochumba na kuipeleka Tanzania fainali.
Amina Bilal ambaye ni kapteni wa Twiga aliibuka mchezaji bora kwenye mechi hiyo na katika mahojiano baada ya
mechi alisema:"Nimepata tuzo kwa sababu ya juhudi zangu na wachezaji wenzangu, kipindi chapili mchezo ulikuwa
mgumu kwa sababu tulishasomana."