Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Oscar anapiga dili kimtindo

Oscar Joshua

Muktasari:

Miongoni mwa wachezaji walioangukiwa na neema hiyo ya usajili wa fedha si haba ni beki wa kushoto wa Yanga, Oscar Joshua, ambaye anakiri klabu yake imeweza kumbadilishia maisha yake tangu alipojiunga nayo mwaka 2010 akitokea Ruvu Shooting.

KWA Tanzania, Azam FC,Simba na Yanga ndiyo klabu za kwanza za soka kuwa na uwezo wa kusajili mchezaji hata kwa Sh80 milioni bila kuathiri shughuli nyingine klabuni.

Miongoni mwa wachezaji walioangukiwa na neema hiyo ya usajili wa fedha si haba ni beki wa kushoto wa Yanga, Oscar Joshua, ambaye anakiri klabu yake imeweza kumbadilishia maisha yake tangu alipojiunga nayo mwaka 2010 akitokea Ruvu Shooting.

Mpaka sasa, Joshua mwenye taaluma ya uandishi wa habari, anakiri maisha yake kiuchumi yamebadilika kwa kiasi kikubwa kwani anaishi kwa kufuata misingi mizuri ya matumizi aliyojiwekea tangu mwanzo.

“Siyo siri Yanga sitaisahau katika maisha yangu kwani imenipa heshima kubwa ndani na nje ya nchi, kwani wachezaji wengi wenye majina makubwa wamepitia katika timu hii na kupata urahisi wa mafanikio na kujulikana Afrika Mashariki na Kati,” anasema Joshua.

Dili zake

Tofauti na Danny Mrwanda anayerejea Vietnam kucheza soka la kulipwa ambaye anamiliki biashara za daladala jijini Dar es Salaam, Joshua yeye anafanya biashara ya kusafirisha na kuuza kompyuta mpakato ‘Laptop’.

Huo ni mradi mmoja kati ya kadhaa aliyonayo ambayo aliianzisha baada ya kupata fedha za usajili Yanga na posho mbalimbali anazopata klabuni hapo na timu ya Taifa, Taifa Stars.

“Mafanikio niliyoyapata Yanga yananifanya kuwa na mtazamo wa kuona mbali zaidi kimaisha tofauti na wakati nacheza katika klabu nyingine, sasa nafikiria mambo makubwa ambayo yatanisaidia kusukuma maisha yangu baadaye,” anasema Joshua.

Joshua anakiri Yanga kumwezesha kukutana na wadau mbalimbali na waliofanikiwa ambao wanampa mwongozo katika biashara sasa hivyo kuwa na msingi mzuri wa maisha. Beki huyu hununua Laptop jijini Dar es Salaam na kwenda kuziuza Mwanza ambako anakiri kuwa na soko zuri la biashara hiyo.

Tofauti wa timu zingine na Yanga

Joshua anasema tofauti na timu nyingine, Yanga usajili wao ni makini kwa kila safu kwani husajili wachezaji wenye ushindani mkali wa kuwania nafasi na hakuna ambaye anapenda kukaa benchi, kitu kinachoongeza chachu ya ushindani kikosini.

Pamoja na hilo anaelezea kuwa uongozi wa Yanga upo makini kuhakikisha wachezaji wao wanawapa mishahara yao inayolingana na kazi wanazozipata pia kupewa kwa kuwapa mishahara yao kwa wakati, jambo linalowafanya kuwapa urahisi wa kufanya mambo ya kimaendeleo.

“Mchezaji ukitaka afanye vizuri uwanjani mpe mshahara wake kwa wakati anakuwa anajituma kwa bidii kwa sababu kila mwisho wa mwezi anajua ana kitu anachokitarajia tofauti anapokuwa anasumbuliwa kupewa haki yake kwani hatoweza kufanya vizuri kulingana na kwamba anakuwa kwenye wakati mgumu,” anasema.

Amepitia kwa makocha wataalamu

Joshua ni miongoni mwa wachezaji wachache waliopata bahati ya kufundishwa na makocha wengi wa kigeni katika kikosi cha Yanga, mpaka sasa amefundishwa na makocha sita na kupata uzoefu mkubwa.

“Sasa najua mchezaji anatakiwa kufanya kitu kipi kwa kocha kwani ninajua falsafa zao kupitia hao sita waliowahi kunifundisha, wote hao wanapenda kila jambo liende kwa wakati na mchezaji akishindwa kufanya hivyo anaonekana ni mtovu wa nidhamu,” anasema.

Makocha hao ni Kostadin Papic (Serbia), Sam Timbe (Uganda), Tom Saintfiet (Ubelgiji), Ernie Brandts (Uholanzi), Hans van Der Pluijm (Uholanzi) na sasa Marcio Maximo wa Brazil.

“Kila kocha ana mbinu zake, hizo zote kwangu zimekuwa na manufaa ya hali ya juu, jambo hilo limekuza kiwango changu,” anasema Joshua.

Ushindani wa namba

Katika kikosi cha Yanga, Joshua anakumbana na ushindani wa namba kwani kila mchezaji anapenda kucheza ili aonekane na kukuza thamani yake aweze kufika mbali zaidi, hilo linamfanya Joshua ajitume kikamilifu.

Katika nafasi yake, anashindana na Edward Manyama, lakini yeye amebahatika kujipatia namba ya kuaminika katika kikosi cha kwanza.

“Si kazi rahisi kupata namba katika kikosi cha kwanza kwa sababu uamuzi wa mwisho upo kwa kocha nani anamuhitaji katika mechi husika,” anasema beki huyo.

Hatosahau kipigo cha Mtibwa

“Kati ya mambo magumu kwangu msimu huu ni siku niliyoumia katika mechi ya ufunguzi dhidi ya Mtibwa Sugar, tuliyofungwa mabao 2-0, kwani nilikuwa naugulia maumivu ya kufungwa na kuumia pia”, anasema.

Katika mchezo huo uliochezwa Septemba 20 pale Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, Joshua aliumia nyama za paja na kufanyiwa mabadiliko.

Baada ya mchezo huo, akawa ana maumivu mara mbili yaani nyama za paja na kipigo kutoka kwa Mtibwa. Pia anaeleza kuwa ligi msimu huu imekuwa haitabiriki katika matokeo jambo hilo linawafanya waumize kichwa katika kila mechi wanayocheza.

Joshua pia amejihakikishia nafasi katika kikosi cha Taifa Stars ambako anacheza namba tatu yaani beki wa kushoto na mara zote Kocha Mart Nooij humtumia kama ilivyo katika kikosi cha Yanga.