Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ndumbaro: Kriketi  dunia wanafuzu Dar

Ndumbaro Pict
Ndumbaro Pict

Muktasari:

  • Mashindano hayo kwa sasa yanafanyika kwenye viwanja viwili, Uwanja wa Dar es Salaam Gymkhana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, yakishirikisha nchi sita ambazo ni Cameroon, Ghana, Malawi, Lesotho, Mali, na wenyeji Tanzania.

SERIKALI imesema kuwa Tanzania imepiga hatua kubwa katika mchezo wa kriketi kiasi cha kuaminiwa kuandaa mashindano ya kufuzu Kombe la Dunia kwa upande wa Afrika, yajulikanayo kama ICC Men’s T20 World Cup Sub Regional Africa Qualifier A.

Mashindano hayo kwa sasa yanafanyika kwenye viwanja viwili, Uwanja wa Dar es Salaam Gymkhana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, yakishirikisha nchi sita ambazo ni Cameroon, Ghana, Malawi, Lesotho, Mali, na wenyeji Tanzania.

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Damas Ndumbaro, alisema kuwa siyo kazi rahisi kupewa dhamana ya kuandaa mashindano hayo, ambapo timu mbili za kwanza zitafuzu katika fainali hizo.

“Tunajivunia sana kuwa wenyeji wa Mashindano ya ICC Men’s T20 World Cup Sub Regional Africa Qualifier A. Hii ni hatua muhimu kwa kriketi nchini Tanzania na inaonyesha dhamira yetu ya kuendeleza mchezo huu kwenye kiwango cha juu zaidi,” alisema Ndumbaro.

Alisema dira ya serikali ni kila mchezo upate maendeleo makubwa na kuitangaza nchi nje ya mipaka kupitia ushindi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Kriketi Tanzania (TCA), Sree Kumar, alisema kuwa ICC imewapa jukumu la kuandaa mashindano hayo kutokana na hatua kubwa ya maendeleo ambayo Tanzania imepiga mpaka sasa.

Kumar alisema wanajivunia sana kupewa fursa ya kuonyesha ukarimu, utamaduni, na maendeleo ya kriketi nchini Tanzania, Afrika, na dunia kwa ujumla.

Aliongeza kuwa fursa nyingine ni kwa wachezaji ambao wataonekana kimataifa, kwani michuano hiyo inaonyeshwa duniani kote kupitia vyombo mbalimbali vya mitandaoni pamoja na ICC.

Aliipongeza serikali ya Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwa mstari wa mbele kuendeleza michezo nchini.

 “Serikali yetu inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan inaamini kwamba michezo ni muhimu kwa ukuaji wa taifa letu,” alisema Kumar.

“Dira yake na kujitolea kwake kukuza michezo vimetupa msingi wa kuendeleza kriketi nchini Tanzania. Tunashukuru kwa sapoti yake na kutuma hamasa kubwa.” Kumar pia alimshukuru Ndumbaro kwa msaada uliofanikisha mchezo huo kufanikiwa kuvutia mashabiki wengi.

Alisema TCA ina malengo makubwa kupitia mchezo wa kriketi ikiwa kuanzisha programu za vijana na kushiriki katika mashindano mbalimbali ya kimataifa.

“Tanzania kwa sasa tuna vijana wenye vipaji ambao wanacheza Kiriketi, huu ni mpango mkakati wetu ambao umanza kuleta matokeo chanya,” alisema Kumar.