Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ndanda yaipiga mkwara Mbuni

Ndanda yaipiga mkwara Mbuni

Muktasari:

  • Timu ya Mbuni FC inafungua rasmi pazia la msimu wa Ligi daraja la kwanza (championship) dhidi ya wageni wao Ndanda FC kutoka Mtwara leo jioni saa 10:00 katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha.

Arusha. Timu ya Ndanda FC 'wanakuchere' imempiga mkwara mpinzani wake Mbuni FC kuelekea mchezo wao unaotarajiwa kuchezwa katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha.

Ndanda wamepiga mkwara huo ikiwa zimesalia saa chache kufika saa 10:00 jioni kuvaana na wenyeji wao Mbuni katika mchezo wa awali wa ufunguzi wa ligi daraja la kwanza inayoanza Leo  jumamosi katika viwanja mbali mbali nchini.

Akizungumza jijini Arusha kocha wa Ndanda, Shaweji Nawanda alisema ingawa wana uchovu wa hali ya juu kutokana na kuchelewa kufika Arusha lakini hakuna cha kuwazuia kuhakikisha wanavuna alama tatu dhidi ya wenyeji wao Mbuni.

"Mbuni tunawafahamu ingawa hatujawahi kukutana nao katika ligi na tunawaheshimu sana hivyo tutacheza nao kwa tahadhari kubwa ili kupata matokeo." alisema Nawanda.

Kocha Nawanda amesema kuwa wametua Arusha na kikosi cha wachezaji 22 wenye afya njema, ari na kiu ya mchezo na matokeo .
Alisema kuwa man'dhari ya Arusha inawapa kiburi zaidi kutokana na hali ya hewa ya ubaridi iliyoko, lakini pia uwanja wa Sheikh Amri Abeid wenye maboresho makubwa sambamba na  maandalizi ya timu yao.

"Maandalizi makubwa na hali ya kikosi itatupatia matokeo kwani tumewatengeneza vijana na tumewaandaa wavuna walichofuata hivyo niwaalike watu wa Mtwara walioko Arusha waje kushuhudia timu yao iko hapa." alisema Nawanda.
"Hatujawahi kukutana na Mbuni lakini kwa sababu tuna timu nzuri naamini hakuna kinachoshindikana ndani ya Dakika 90 mtaona wenyewe na nitumie nafasi hii kuwamba wana Mtwara waendelee kuiombea timu yao wawaletee walichowatuma."