Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mzize awapiga chini Feisal, Dube

Muktasari:

  • Katika taarifa iliyotolewa na kamati hiyo imesema Mzize aling’ara kwenye mwezi huo akiwashinda Prince Dube na Feisal Salum wa Azam FC alioingia nao kwenye fainali katika mchakato wa tuzo hizo.

Kamati ya tuzo za TFF imemchagua kocha wa Yanga, Sead Ramovic kuwa kocha bora wa mwezi Desemba wa Ligi Kuu Bara huku pia ikimchagua mshambuliaji wa timu hiyo Clement Mzize kuwa mchezaji bora wa mwezi huo .

Katika taarifa iliyotolewa na kamati hiyo imesema Mzize aling’ara kwenye mwezi huo akiwashinda Prince Dube na Feisal Salum wa Azam FC alioingia nao kwenye fainali katika mchakato wa tuzo hizo.

Mzize alihusika kwenye ushindi wa mechi nne za Yanga akicheza dakika 288 huku akifunga mabao manne na kuhusika kwenye mengine matatu na timu hiyo kukaa katika nafasi ya pili ya msimamo wa Ligi Kuu Bara.

Kwa upande wa Ramovic yeye amewashinda Fadlu Davis wa Simba na Rachid Taoussi wa Azam FC, aliiongoza Yanga kushinda michezo minne na kushinda yote na kuivusha timu hiyo kutoka nafasi ya tatu hadi ya pili, akishinda mbele ya Tanzania Prisons 4-0, Dodoma Jiji 4-0, Mashujaa 3-2 na dhidi ya Fountain Gate kwa mabao 5-0.

Aidha kamati imemchagua meneja wa JKT Tanzania Ashraf Omar kuwa meneja bora wa Uwanja wa mwezi Desemba akisimamia uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo akifanya vizuri katika menejimenti ya matukio ya michezo pamoja na masuala yanayohusu miundombinu ya uwanja.