Mo Dewji: Hans Poppe ulikuwa wa kwanza na ulinyooka linapokuja suala la kuilinda Simba

Kufuatia kifo cha aliyekuwa Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi Simba, Zakaria Hans Poppe, Mohammed Dewji ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo ameandika haya;

"Moyo wangu una maumivu makali sana. Bado ni vigumu kuamini na kukubali kuwa mjumbe wetu, kaka yetu, Zakaria Hans Poppe hatunaye tena,

"Kaka yangu, nimefanya kazi na wewe kwa miaka mingi, na kila siku uliweka maslahi ya Simba mbele. Kaka yangu ulikua na wema wa kipekee, na ulikua wa kwanza na ulinyooka linapokuja suala la kuilinda Simba, hukuwa na maslahi binafsi. Ulikua rafiki wa marafiki wa Simba, na ulikua tofauti na wasioitakia mema Simba,"

"Kaka yangu, Umetangulia nasi tutafuata. Nitakukumbuka sana kaka yangu. Natoa pole sana kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki, pamoja na wanafamilia wote na mashabiki wa Simba kwa kumpoteza ndugu yetu. Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi,".