Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mnyamisi afichua mipango mipya Bigman FC

MNYAMISI Pict

Muktasari:

  • Msimu wa 2024-2025, nyota huyo aliiwezesha TMA kumaliza Ligi ya Championship nafasi ya tano na pointi 53, ingawa msimu huu hadi sasa Bigman FC inashika nafasi ya nane na pointi 27, baada ya kushinda saba, sare sita na kupoteza tisa.

BEKI wa kati wa Bigman FC, Better Abdallah Mnyamisi amesema malengo ya timu hiyo kwa sasa ni kupigania nafasi ya kubaki Ligi ya Championship msimu ujao, baada ya waliyoweka awali kuonekana ni ngumu Zaidi kuyatimiza.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mnyamisi amesema alijiunga na kikosi hicho dirisha dogo la Januari 2026 na malengo aliyokuta kwa viongozi, benchi la ufundi na wachezaji wenzake ni kumaliza pia nafasi nne za juu katika msimamo.

"Kwa tulipo sasa ni ngumu kusema tunamaliza nafasi nne za juu ambayo itatupa fursa ya kucheza mechi za mtoano, kwa mechi zilizobakia na ushindani uliopo kutoka kwa wapinzani wetu, ni ngumu sana kutimiza hilo," amesema Mnyamisi.

Nyota huyo aliyejiunga na Bigman FC Januari 2026 akitokea IAA SC baada ya kuachana na TMA ya Arusha inayoshiriki Ligi ya Championship, amesema kwa sasa ataendelea kukipambania kikosi hicho ili kitimize malengo ya kubakia msimu ujao.

Nyota huyo licha ya kucheza Championship msimu wa 2024-2025, ila ana uzoefu mkubwa pia wa kucheza Ligi Kuu Bara na aliwahi kuitumikia Polisi Tanzania kuanzia msimu wa 2021-2022 hadi 2023-2024, kisha akajiunga rasmi na TMA.

Msimu wa 2024-2025, nyota huyo aliiwezesha TMA kumaliza Ligi ya Championship nafasi ya tano na pointi 53, ingawa msimu huu hadi sasa Bigman FC inashika nafasi ya nane na pointi 27, baada ya kushinda saba, sare sita na kupoteza tisa.