Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Messi aitwa baba, Ronaldo yeye na mademu damudamu

Muktasari:

Messi anakuwa mwingi wa hisia pale anapomzungumzia mwanaye Thiago, mafanikio yake yote, mataji na rekodi alizoweka hayakuwa na mlinganio wowote na Ijumaa ya Novemba, 2012, saa 11:14 jioni alipozaliwa Thiago katika Hospitali ya USP Dexeus karibu na Nou Camp.

KATIKA toleo, mwandishi Luca Caioli alizichambua tabia za Ronaldo anayezungumzwa ni mpenda mademu tofauti huku Messi akihusishwa na mwanamke mmoja tu wa tangu utotoni. Sasa endelea…

Linapokuja suala la wanawake Ronaldo anasema anapenda tabasamu zuri, mvuto wenye kuhamasisha, uungwana na mazungumzo yanayovutia.

“Kucheka ni kati ya mambo ya kunisaidia kupoteza muda,” anasema ingawa anasema hapo hapo tusisahau mwonekano mzuri jambo ambalo lina umuhimu sana ingawa muhimu zaidi ni kile kilicho ndani hata kama mwanamke ana uzuri wa kipekee kama Angelina Jolie.

“Nimebadilika, ni suala la kimtazamo, hilo ndilo linalokuja mwanzo na mengine yote yanafuata, imenibadili mtazamo wangu kuhusu mechi, hapo kabla inapotokea tumepoteza mechi au mimi kucheza vibaya nisingezungumza na mtu kwa siku tatu au nne ili tu kutuliza hasira zangu.

“Lakini kwa sasa kama nikipoteza mechi ninakwenda nyumbani na kumwona mtoto wangu baada ya hapo nasahau yote yaliyopita, naweza kuwa na hasira moyoni lakini nikimwona mtoto wangu kila kitu kinabadilika.

“Kitendo cha kuwa baba kimenisaidia kuwa mtu mzima, imenisaidia kupunguza hulka ya kutekwa na soka kulikopitiliza na kuamini kuna mambo mengine katika maisha pia.

Messi anakuwa mwingi wa hisia pale anapomzungumzia mwanaye Thiago, mafanikio yake yote, mataji na rekodi alizoweka hayakuwa na mlinganio wowote na Ijumaa ya Novemba, 2012, saa 11:14 jioni alipozaliwa Thiago katika Hospitali ya USP Dexeus karibu na Nou Camp.

Mdogo wake Messi, Maria Sol ndiye aliyepewa jukumu la kuiarifu dunia kuhusu ujio huo mpya, nusu saa baada ya mtoto huyo kuzaliwa, Maria aliandika kupitia Twitter, “Karibu duniani mtoto Thiago!! Messi sasa baba.”

Maria ndiye aliyemsindikiza Antonella kwenye wodi ya wazazi saa tatu asubuhi katika jengo kwenye ghorofa ya saba, sehemu ambayo familia itapata nafasi ya kuwa huru bila kuingiliwa mambo yao binafsi.

Jorge, Celia, Matias, Rodrigo na Maria Sol aliwasili saa tisa alasiri wakati Messi akiwa pembeni ya Antonella akimsaidia kwa kila kitu.

Kila kitu kilikwenda vizuri na mama na mtoto wote walikuwa wazima wa afya, saa 12 na dakika 20 jioni, Messi naye akatuma ujumbe kupitia mtandao wa Facebook,

“Leo mimi ni mtu mwenye furaha zaidi duniani, mwanangu amezaliwa na namshukuru Mungu kwa zawadi hii! Naishukuru familia yangu kwa msaada wao, shukrani wote.

Ujio wa Thiago pia ulikuja na mabadiliko mengine. Messi alionekana muwazi na asiye na hofu kuwapa watu taarifa hiyo na baada ya mtoto huyo kuzaliwa alikwenda uwanjani akiwa na nia ya kulifikisha jambo hilo kote duniani kwa kulitoa zawadi kwa mwanaye bao alilofunga baada ya mtoto huyo kuzaliwa.

Tayari alishalisema hilo saa chache kabla, “Nitafanya kitu cha kipekee nitakapofunga bao la kwanza lakini baada ya hapo nitarudi katika hali ya kawaida. Hata hivyo, pamoja na juhudi zote alizozifanya hakuweza kupata bao katika mechi dhidi ya Celta Vigo na badala yake alilazimika kusubiri hadi Novemba 7 katika mechi dhidi ya Celtic.

Alifunga katika dakika za majeruhi na kuweka kidole gumba mdomoni kuashiria kupata mtoto na alipoulizwa ni kwa nini alifanya tukio hilo ambalo halikuwa kubwa na lenye kuvutia alisema, “Bao halikuwa na maana sana kwani Barca iliishia kufungwa mabao 2-1, kukawa na nafasi nyingine nyingi ya kutoa heshima ya bao kwa mtoto wake.”

Jumapili ya Novemba 11 katika mechi ya La Liga dhidi ya Mallorca, Messi alipata nafasi ya kushangilia mabao yake mawili ya ushindi pamoja na kuzaliwa kwa mtoto wake katika namna ambayo aliitaka.

Jumapili ya Novemba 25 katika mechi dhidi ya Lavante alivaa kitambaa kidogo mkononi kilichokuwa na maandishi yaliyosomeka, I love Thiago, alibusu kwenye kitambaa hicho kwa kila bao alilofunga.

“Thiago ni muhimu mno katika maisha yangu, wakati wote nitamweka mbele, hakuna shaka ni zawadi bora ambayo kila mtu angependa kuipata.”

Itaendelea Jumamosi ijayo…