Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbadala wa Pinto kujulikana Novemba 5

Muktasari:

Maazimio ya kufanya uchaguzi huo, yamepitishwa  baada ya kamati ya utendaji ya chama hicho kukutana jana Jumatano.

Dar es Salaam. Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (Taswa) kinatarajia kufanya uchaguzi Novemba 5 mwaka huu.
Maazimio ya kufanya uchaguzi huo, yamepitishwa  baada ya kamati ya utendaji ya chama hicho kukutana jana Jumatano.
Mwenyekiti wa chama hicho, Juma Pinto amesema, uchaguzi huo utashirikisha Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kwa ajili ya usimamizi wa karibu na watakaotakiwa kupiga kura  ni wale walio katika leja kuanzia Juni 20o7.
"Kikao kimekubaliana watakaoshiriki uchaguzi huo ni wanachama wote wa Taswa waliopo katika leja kuanzia Juni mwaka 2007 hadi Juni mwaka 2017, wakiwemo walioingia uanachama wakati wa semina ya waandishi chipukizi iliyofanyika Dar es Salaam Agosti mwaka 2015 na sharti kubwa ni kila mwanachama kulipia ada ya mwaka mmoja,"alisema Pinto.
"Kwa wanachama wengine wapya wanaotaka kujiunga, watafanya hivyo baada ya uongozi mpya kuingia madarakani na kupewa utaratibu kulingana na Katiba ya chama inavyoeleza na pia kwa kadri uongozi mpya utakaoingia madarakani utakavyoona inafaa."
Uongozi unaomaliza muda wao tangu walipochaguliwa  mwaka 2014,  Mwenyekiti ni Juma Pinto, Egbert Mkoko alichaguliwa Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu ni Amir Mhando na msaidizi wake ni Grace Hoka.
Shija Richard alichaguliwa nafasi ya  Mhazini na Zena Chande ni Mhazini Msaidizi na wajumbe ni pamoja na Rehure Nyaulawa, Chacha Maginga, Mussa Juma, Mwani Nyangassa, Mroki Mroki, Ibrahim Bakari na Majuto Omary kupitia nafasi yake ya Mwenyekiti wa Taswa FC.