Mashabiki Simba wamkosha Lwanga

Wednesday July 21 2021
lwanga pic
By Clezencia Tryphone

KIUNGO wa Simba, Taddeo Lwanga amesema kwa namna ambavyo watanzania wanapenda mpira wanakazi kubwa msimu ujao kuhakikisha wanatetea tena ubingwa.
Simba imetwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara mara nne mfululizo huku sasa ikisaka utetezi wa kombe la FA Julai 25 mkoani Kigoma.
Kwa mujibu wa Lwanga amependa namna ambavyo mashabiki wanapenda mpira na kujitokeza viwanjani kuzipa sapoti timu zao.
Amesema namna ambavyo wanajitoa ni deni kubwa kwao kuhakikisha wanafanya vizuri katika ligi na michuano ya Kimataifa.
"Sijawahi kuona mashabiki wanajaa hivi uwanjani, ni mapenzi ya dhati kwa timu zao na hata sisi wachezaji ni jukumu letu kuhakikisha tunafanya vizuri katika michezo yetu yote tunayocheza," alisema Lwanga.
Kutua kwa Lwanga ndani ya kikosi hicho kulipelekea mzawa Jonas Mkude aliyekuwa chagua la kwanza ndani ya timu hiyo kupata wakati mgumu wa kuanza msimu huu.

Advertisement