Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Makonda awapa Yanga ng’ombe watano, Simba ikiambulia mmoja

Muktasari:

  • Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda ametekeleza ahadi yake kwa kutoa ng’ombe watano kwa Yanga na mmoja kwa Simba, aliyoitoa siku chache kabla ya kuchezwa mchezo wa dabi uliofanyika Novemba 05,2023.

Dar es Salaam. Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Paul Makonda, ametimiza ahadi iliyotolewa siku chache kabla ya kufanyika kwa mchezo wa dabi ya Kariakoo, inayozihusu timu za Simba na Yanga.

Katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara (NBC), uliofanyika siku 19 zilizopita na kuhitimishwa kwa mwenyeji Simba kukubali kichapo cha mabao 5-1 dhidi ya Yanga, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Makonda aliahidi katika kila bao moja atatoa ng’ombe mmoja.

Ahadi hiyo, imekabidhiwa leo Ijumaa, Novemba 24, 2023 Makao Makuu ya Klabu ya Yanga na Katibu Msaidizi Mkuu, Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo ya CCM, Shaibu Akwilombe kwa niaba ya Makonda na kupokelewa na Mkurugenzi wa Sheria wa Yanga, Simon Patrick.

Akizungumza kwenye makabidhiano ya ng’ombe hao, Akwilombe aliyeonekana mwenye furaha na tabasamu huku akisema: “Tumekutana leo, kutekeleza ahadi yetu iliyotolewa siku chache kabla ya mchezo wa watani wa jadi...kwenye gari kuna ng’ombe sita, watano nakabidhi Yanga na mmoja naenda kukabidhi Simba.”

“Ahadi ilitolewa na mkuu wa Idara yetu ya Itikadi, Paul Makonda. Aliahidi katika kila goli litakalofungwa atatoa zawadi ya ng'ombe katika mchezo ule Yanga walishinda goli tano na Simba walipata bao moja," amesema.

Kwa upande wake, Wakili Patrick amemshukuru Makonda kwa kutekeleza ahadi yake kwa kuwapatia zawadi ya ng’ombe wa tano kama alivyowaahidi.

“Aliahidi bao lolote litakalofungwa kwenye mchezo dhidi ya Simba na Yanga atatoa ng’ombe mmoja kwa maana hiyo tumekabidhiwa ng’ombe watano ishara ya kufunga mabao matano," amesema.

Patrick amemuomba kiongozi huyo na wengine kuendelea kuwaunga mkono kwenye michezo yao inayokuja huku akieleza kikosi chao siku ya leo kinatarajiwa kucheza mchezo mgumu dhidi ya CR Belouizdad ya Algeria mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Mchezo ni mgumu, tumuomba kupitia uongozi wake tunaomba ahadi hii iendelee ilikuendelea kutoa hamasa kwa wachezaji lakini hawa ng’ombe watano tumewapokea viongozi tutajadiliana na tutajua cha kuwafanyia tutawatangazia,” amesema.

Akishukuru kwa niaba ya wazee wa Klabu ya Yanga, David Katundu amesema: “Mabao matano yamekuwa chanzo cha mpatanishi kwa watani wetu wa jadi Simba bila kuwapiga hizo wasingejua wana upungufu gani, ni jambo jema na nzuri.”