Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Makocha wasaka mbinu kumdhibiti Pep Guardiola

Muktasari:

  • “Unawaangalia wachezaji machoni na inakuwa kama vile unamuangalia mpenzi wako, unaona hamasa na utayari wa kuhamasishwa au unaona hamasa imeondoka, kitu hicho hicho kinaweza kutokea hapa Bayern.

KATIKA toleo lililopita kwenye kitabu cha Pep Confidential, Mwandishi Marti Perarnau katika mazungumzo yake na Kocha Pep Guardiola, kocha huyo aligusia kipindi kigumu cha kuhamasisha wachezaji hasa unapoona dalili ambazo hazitoi picha nzuri kutoka kwa wachezaji wako. Endelea…

“Unawaangalia wachezaji machoni na inakuwa kama vile unamuangalia mpenzi wako, unaona hamasa na utayari wa kuhamasishwa au unaona hamasa imeondoka, kitu hicho hicho kinaweza kutokea hapa Bayern.

“Baada ya miaka michache ijayo, nitakuwa tena sina ule uwezo wa kuwahamasisha wachezaji wangu na huo utakuwa wakati wa kuondoka, kila kitu kitakuwa kikionekana machoni, hapo ni suala kubwa ni uwezo wa kuhamasisha wachezaji.

Kama mwezi Machi ulikuwa wa maajabu kwa Bayern, basi mwezi Aprili ulikuwa ni majanga, wakiwa tayari na taji la ligi mkobani, Pep anafanya mabadiliko katika mechi dhidi ya Hoffenheim.

Thiago alihitaji kucheza kwa sababu katika wiki mbili zilizopita alicheza mechi chache, kwa sababu alichubuka vibaya mguu, kwa hiyo anahitaji haraka kurudi katika kasi yake ambayo ilimfanya awe mtu muhimu kwenye timu katika kipindi cha Januari na kuendelea.

Kwa hiyo, alikuwa katika kikosi cha kwanza pale Allianz Arena kwa sababu Pep pia anataka awe katika kikosi cha kwanza kwenye mechi ya jijini Manchester dhidi ya Man United siku chache zilizofuata.

Hata hivyo, dakika 10 baada ya mechi Thiago anapata maumivu wa misuli, mwamuzi anapuliza filimbi kuashiria faulo lakini wakati mechi ikiendelea, Thiago anajiweka katika mazingira hatarishi, anajilegeza na kuumizwa na Kevin Vollan, kosa kubwa. Mguu wake anahitaji matibabu makubwa.

Siku iliyopita Pep alikataa ofa mbili, ya kwanza ya kununua beki wa kati maarufu, hakuamini katika kubadili mbinu aliyokuwa nayo, hivyo na wazo hilo akalikataa, ofa nyingine ni ya ahadi ya pesa lukuki kuongezwa katika mshahara wake kama angetwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya mwishoni mwa msimu. Kwa hulka yake alikataa jambo hilo pia.

Hii ni siku ambayo aliamua kufunga ukurasa wa ligi ambayo tayari alishabeba taji lake na hapo akatangaza, “Kwa heshima ya ligi hii ya Bundesliga tutaendelea kupambana kwa bidii lakini Jumanne tuna ‘fainali’ mjini Manchester, ndio wanaiita robo fainali lakini ni fainali kwa sababu tumebakiwa na mechi tatu tu za ushindani, mbili dhidi ya Manchester na fainali ya DFB-Pokal dhidi ya Kaiserslautern.

“Kwa sasa kuweka rekodi hakuna maana yoyote badala yake jambo la muhimu kwangu ni kushinda hizi mechi tatu tu.”

Kwa maneno hayo ni wazi anachotumaini Pep ni kufunga ukurasa mmoja na kufungua wa pili yaani malengo ya Bundesliga yalifikia mwisho, nguvu zote sasa alizielekeza kwenye kusaka mataji mawili yaani Ligi ya mabingwa na DFB-Pokal. Hakutaka kabisa fikra za wachezaji wake ziwe katika mambo ya kawaida ya kuweka rekodi.

Mpango wake huuhuu ndio uliosababisha anguko la kiwango cha uchezaji kwa wachezaji wake, ni kama mbegu ambayo ilianza kuchanua na kuwafanya wachezaji waliokuwa na furaha kuwa kama walio kwenye majanga.

Hoffenheim walicheza soka la kasi na kuisumbua Bayern, na hilo liliwaweka katika wakati mgumu wachezaji wa Bayern wengi wao wakiwa ni wale wa akiba kina Starke, Van Buyten, Contento, Pizarro, Shaqiri.

Katika wiki chache zilizopita timu za Nuremberg, Mainz na Wolfsburg ziliwapa presha mabeki Bayern kwa kupandisha mashambulizi mara kwa mara wakati Bayern ikicheza kuanzia nyuma lakini mwisho wa siku timu ya Pep ilifanikiwa kushinda mechi zote hizo. Hata hivyo, pamoja na ushindi huo baadhi ya makocha wa Ujerumani wakiwamo kina Markus Weinzierl wa Augsburg, Thomas Tuchel wa Mainz 05 na Dieter Hecking wa Wolfsburg hawa walianza kutafuta mikakati ya kuzikabili mbinu za Pep hasa aina ya uchezaji.

Hoffenheim waliwasumbua mno Bayern kiasi kwamba Bayern ikalazimika kubadili aina ya uchezaji wake na kuanza kutegemea mashambulizi ya kushitukiza jambo ambalo lilikuwa la kushtusha hasa pale matokeo ya mwisho yaliposomeka kuwa ni sare ya mabao 3-3.

Itaendelea Jumanne ijayo…