Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Lahm, Hojbjerg kielelezo tosha cha falsafa za Pep

Muktasari:

Lahm: Umakini wake na uelewe katika mbinu za kiuchezaji ndiyo nguvu yake kubwa, lakini pia yuko makini katika kila kitu anachokifanya na anatuandaa vizuri kwa kila timu pinzani, ni kocha bora na pengine hiyo inaweza kuwa ni udhaifu mdogo kwa sababu ni mfano wa mtu aliyekamilika.

TOLEO lililopita kwenye Kitabu cha Pep Confidential, Mwandishi Marti Perarnau aliendelea na mazungumzo yake na mchezaji Philipp Lahm wa Bayern na jambo moja ambalo Lahm alilizungumzia ni sifa ya Pep kuwa makini kwa kila jambo huku akiwa si mwenye kubweteka baada ya kuulizwa kuhusu uzuri na ubaya wa Pep. Endelea…
Perarnau: Ni mambo gani mazuri na mabaya kuhusu Pep?
Lahm: Umakini wake na uelewe katika mbinu za kiuchezaji ndiyo nguvu yake kubwa, lakini pia yuko makini katika kila kitu anachokifanya na anatuandaa vizuri kwa kila timu pinzani, ni kocha bora na pengine hiyo inaweza kuwa ni udhaifu mdogo kwa sababu ni mfano wa mtu aliyekamilika.
“Anataka kila kitu hadi kile kidogo cha mwisho, anataka awe mkamilifu kwa kila kitu, hilo ni jambo zuri kwa jinsi mambo yanavyokwenda lakini kuna wakati anakwenda mbali zaidi na kumzuia asiwe mtu mwenye kuridhika na hatua aliyofikia, hajawahi kujiruhusu kukaa chini kubweteka na kusema hii sasa kila kitu safi, ni mwanzo mwisho.
Perarnau: Je, unadhani ataweza kudumu muda mrefu?
Lahm: Nadhani atadumu muda mrefu ingawa hilo pia litategemea na wachezaji, kwa sababu timu inapokuwa na mafanikio uwezekano wa kocha kukaa muda mrefu ni mkubwa lakini kwa klabu kubwa na ya hadhi ya juu kama Bayern msipopata ushindi wa mara kwa mara hapo kila mtu ataanza kumtilia shaka kocha wakiwamo wachezaji.
“Hata hivyo, bado nina matumaini upo uwezekano wa kuendelea kushinda chini ya Pep, nafurahia kufanya kazi nikiwa chini yake.
Perarnau: Staili yako ya uchezaji inamaanisha wapinzani wenu watalazimika kucheza kwa kujihami zaidi na kusubiri mfanya mashambulizi ya kushitukiza, je, haikuchoshi kwa kuwa mtu wa kucheza kwa staili hiyo kwa wakati wote.
Lahm: Naweza kukwambia inakuwa vipi kwa mtazamo wa mchezaji na ni bora unapocheza ukiwa na mpira kuliko kuwa mwenye kukaba kila wakati, unapokuwa mwenye kukaba kwa namna hiyo mwishowe utakuwa ukigusa mpira kwa sekunde zisizozidi tano ukijaribu kupata bao na baada ya hapo unarudi nyuma kwa ajili ya kujihami kwa mara nyingine.
“Ni jambo zuri kuwa na mpira miguuni mwako, ni kweli upo uwezekano wa kukutana na wachezaji 11 wote wakiwa ‘wamepaki basi’  na hapo kunakuwa na ugumu, ni ngumu kweli lakini ni bora muwe wenye kujibiidisha badala ya kusubiri nafasi yako ijitokeze.
Perarnau: Lakini hata mnaposhambulia mwishowe mnakutana na rundo la mabeki mbele yenu na inakuwa ngumu kupata bao, timu hapo inaweza kufanya nini, kufumua mashuti, kupiga krosi nzuri, suluhisho ni nini pale mnapokuwa mmezibiwa njia au wanapopaki basi?
Lahm: Hapo ni lazima tuwe na umakini wa asilimia zote kwa sababu kila pasi mnayocheza inakuwa na maana kubwa, kadiri mnavyopasiana kwa kasi ndivyo wapinzani wenu wanakuwa na muda mdogo wa kuwa na mpira na kadiri wanavyokuwa na mpira kwa muda mdogo ndivyo mnavyokuwa na nafasi ya kuingia katika eneo lao.
“Na ukweli ni kwamba usahihi katika kila hatua mnayokwenda na mpira inakuwa na umuhimu kwa wachezaji wa timu yenu kuisumbua safu ya ulinzi ya mpinzani wenu.
“Jambo la kuangalia ni kwamba timu yenu inapofika eneo dogo la uwanja lililobaki kwenye upande wa timu pinzani hapo kitu pekee muhimu ni jinsi mnavyojipanga vizuri na kulitumia eneo hilo dogo lililopo, unahitaji wachezaji wanaoelewa ukweli huo, wachezaji ambao ni makini katika mbinu na ambao wakati wote watataka kuwa na mpira.”
Na kwa ufafanuzi huo nawataja Hojbjerg na Lahm kuwa ni kielelezo cha falsafa za Pep. Mchezaji mdogo (Hojbjerg) wa kiungo mwenye umri wa miaka 18 ambaye katika mechi ya fainali ya Kombe la Ujerumani dhidi ya Dortmund alicheza nafasi ya beki wa pembeni pamoja na Lahm, beki wa pembeni mwenye umri wa miaka 30 ambaye Pep amembadili na kuwa kiungo wa msimu tishio na tegemeo katika timu.
Itaendelea Jumamosi ijayo…