Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kumekucha! KenGold yatimua watano kwa mpigo

Muktasari:

  • Katika kufanya maboresho wapo watakaopunguzwa na wengine kuongozwa.

Dirisha dogo la usajili tayari limekwisha kufunguliwa tangu Desemba 15, klabu mbalimbali zimeanza kufanya maboresho ya timu zao ili kuongeza nguvu na kufanya vizuri nmzunguko wa pili wa Ligi.

Katika kufanya maboresho wapo watakaopunguzwa na wengine kuongozwa.

Ikiwa inauelekea mchezo mgumu wa Ligi Kuu Bara leo dhidi ya Simba utakaochezwa kwenye Uwanja wa KMC Complex kuanzia saa 10:00 Jioni, Ken Gold imetangaza kuachana na n yota wake watano.

Nyota hao walioachwa ni:

-Steven Mganga

- Amir Njeru

-Castor Posta

-Adam Uled na

- Salum Idrissa

Hadi sasa KenGold imecheza mechi 14 ikishika nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 6. Imeshinda mechi 1, Sare 3 na kupoteza mechi 10.